Pata taarifa kuu
MISRI-MAUAJi-USALAMA

Sinai: vita ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1973

Wanajeshi kumi na saba na zaidi ya wananamgambo wa kiislamu mia moja wameuawa Jumatano Julai 1 kaskazini mwa eneo la Sinaï, nchini Misri.

Magari ya jeshi la Misri katika Sinaï.
Magari ya jeshi la Misri katika Sinaï. Reuters/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Idadi hii imethibitishwa na msemaji wa jeshi katika taarifa kuhusu mapigano, ambapo ilisemekana kuwa ngome kadhaa za wanajeshi wa serikali zilishambuliwa kwa wakati mmoja mapema saa moja asubuhi Jumatano wiki hii.

Kwa upande wao, wanajihadi wa kundi linaloendesha harakati zake katika eneo la Sinaï, lenye uhusiano na Islamic State, wamekiri kutekeleza mfululizi huo wamashambulizi.

Hakujawahi kuonekana vita vya aina hii katika eneo la Sinaï toka vita vya Misri na Israel vya mwaka 1973. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, zaidi ya “magaidi” 300 walishambulia ngome za wanajeshi wa serikali pembezoni mwa mji wa Cheikh Zuweid karibu na mpaka na Gaza, nchini Palestina. Wanamgambo hao wa kiislamu walikua na silaha tofauti za kivita. Walitumia usafiri wa magari ya aina ya 4DW kwa kuweza kutekeleza mashambulizi hayo.

Ni operesheni ya kijeshi inayoaminika ambayo kundi la wapiganaji wa kiislamu wa eneo la Sinai walitekeleza. Kwa upande wake jeshi, pia, lilitumia uwezo mkubwa dhidi ya mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita F 16 na helikopta. Jimbo la Sheikh Zuweid ni sehemu ya eneo lisilokua na wanajeshi kulingana na Mkataba wa amani na Israeli. Ndege za kivita haziruhusiwi kuvuka eneo la mpaka kwenye mto Suez. Kwa sasa, jeshi na wanajihadi, kila upande unadai ushindi na hakuna chanzo huru kinachoweza kuamua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.