Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa Rais nchini Urusi: Vladimir Putin achaguliwa tena kwa 87% ya kura

Rais Vladimir Putin amechaguliwa tena kwa 87% ya kura katika uchaguzi wa rais nchini Urusi, kulingana na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo. Matokeo haya ambayo bado niya muda yalitolewa kwa msingi wa kura kutoka 80% ya vituo vya kupigia kura zlizohesabiwa. Kama inavyotarajiwa katika uchaguzi huu bila mashaka, mkuu wa Kremlin anaelekea kupata ushindi kamili bila upinzani wowote.

Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mahojiano, mjini Moscow, Machi 12, 2024.
Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mahojiano, mjini Moscow, Machi 12, 2024. AP - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin amewashukuru Warusi kwa kupiga kura katika uchaguzi wa rais ambao ameshinda kwa kiasi kikubwa, kulingana na matokeo ya awali. Rais wa Urusi amebaini kuwa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Urusi yaliyompa ushindi wa wazi yalionyesha "imani" ya Warusi katika utawala wake. "Tuna kazi nyingi madhubuti na muhimu za kukamilisha. Matokeo ya uchaguzi yanaonyesha imani ya raia wa nchi na matumaini yao kwamba tutafanya kila kitu kilichopangwa,” amesema katika hotuba yake iliyopeperushwa kwenye televisheni usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Vladimir amehakikisha kwamba nchi yake haitajiruhusu "kutishwa" au "kukandamizwa".

"Uungwaji mkono muhimu", kulingana na runinga ya Urusi

"Uungwaji mkono muhimu", "ujumuishaji wa ajabu" wa jamii... Televisheni ya Urusi ilizidisha sifa kuu kuelezea ushindi wa mkuu wa nchi, baada ya uchaguzi ambao upinzani ulitengwa baada ya ukandamizaji usio na huruma. Ushindi huu unaashiria rekodi kwa mtu ambaye kila mara alikuwa akipata kati ya 64 na 68% ya kura katika chaguzi zilizopita. Mamlaka hapo awali ilisisitiza kwamba raia wa Urusi lazima "waungane" nyuma ya kiongozi wao, ikionyesha kuwa mzozo wa Ukraine ulioanzishwa na nchi za Magharibi ili kuiangamiza Urusi. Shambulio dhidi ya Ukraine, lililoanzishwa na mkuu wa Ikulu ya Kremlin mnamo Februari 2022 na ambalo halina mwisho licha ya makumi ya maelfu ya vifo, lilikuwa mada kuu ya uchaguzi huo, haswa kwamba mashambulio kwenye ardhi ya Urusi yameongezeka wiki hii.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa Vladimir Putin ni mtu "mlevi wa madaraka" ambaye anataka "kutawala milele". "Ni wazi kwa kila mtu kuwa mtu huyu, kama ilivyotokea mara nyingi katika historia, amelewa tu na madaraka na anafanya kila awezalo kutawala milele," Volodymyr Zelensky amesema katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, akibaini kuwa uchaguzi wa urais nchiniUrusi sio "halali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.