Pata taarifa kuu

Ukraine: 'Kyiv yalaani mashambulizi ya magaidi' ya Urusi

Ukraine iko katika maombolezo, siku moja baada ya shambulio linine mbaya huko Odessa, Ijumaa Machi 15. Watu 20 waliuawa, kulingana na idara ya huduma za dharura, na wengine 73 walijeruhiwa, kulingana na ripoti kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine. Volodymyr Zelensky anazungumza juu ya shambulio lililofanywa kwa kutumia makombora mawili, ambapo shambulio la pili lilipiga "wakati waokoaji na matabibu walipokuwa wakifika kwenye eneo la shambulio hilo."

Waokoaji wakipambana na moto huko Odessa mnamo Machi 15, baada ya shambulio baya la Urusi.
Waokoaji wakipambana na moto huko Odessa mnamo Machi 15, baada ya shambulio baya la Urusi. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine anazungumzia shambulio "la kinyama kabisa". Manispa ya mji wa Odessa, mji mkubwa wa bandari ya kusini, umetangaza siku ya maombolezo Jumamosi hii. Kulingana na jeshi la Ukraine, vikosi vya Urusi vilirusha makombora ya Iskander kutoka Crimea.

Mashambulizi mawili mfululizo kwenye eneo moja, kulingana na idara ya huduma za dharura. Shambulio la kwanza la kombora liliharibu miundombinu ya raia na kusababisha moto. Na waokoaji walipofika na kuanza "kuzima moto, kuondoa vifusi na kutafuta waathiririwa", chanzo hicho kinasema, "adui alitekeleza shambulio lingine la kombora".

Mbinu zilizolaaniwa na Mbunge wa Odessa Oleksiy Hontcharenko, aliyehojiwa huko Odessa, mji wake wa asili. "Urusi, anafikiria, ilitumia mbinu za kigaidi katika shambulio hili. Dakika kumi baada ya shambulio la kwanza, Urusi ilifanya shambulio la pili, kwenye eneo la shambulio la kwanza, kuwashambulia madaktari, watu waliokuwepo kusaidia majeruhi. Ni kama magaidi wote. Na kwa sababu hiyo, watu zaidi ya 20 walifariki na kadhaa kujeruhiwa. "

Inasikitisha sana kwa sasa mjini na watu wameshangazwa na matukio hayo. Wakati wa mwezi uliopita, hili sio shambulio la kwanza wala la pili, ni karibu kila siku shambulio jipya dhidi ya jiji letu.

Miongoni mwa waathiririwa, viongozi kadhaa wa kisiasa na kijeshi, akiwemo naibu meya wa zamani ambaye alikua mwanajeshi, na mkuu wa zamani wa polisi wa mkoa. Mahali pa mkutano wao bila shaka palifichuliwa kwa vikosi vya Urusi na maafisa wa ndani, kitendo ambacho kinamsikitisha Oleksiy Hontcharenko.

"Kwa bahati mbaya, kuna mafisa hawa wa Urusi," amesema. Kwangu, ni jambo la kushangaza kwamba watu wanaoishi Odessa wanaweza kumsaidia adui kushambulia miji wanamoishi. Ni jambo la kushangaza, lakini kwa bahati mbaya kuna maafisa hawa wa Urusi. Idara yetu ya usalama inajitahidi kufanya kazi kuwakamatamaafisa hawa na kuzuia hili lisitokei, lakini shambulio hili linaonyesha kuwa maafisa hawa wanafanya kazi. "

"Odessa ni jiji la kimkakati zaidi nchini Ukraine kwa Urusi," anahitimisha mbunge huyo. Na kwa sababu ya thamani hiyo ya kimkakati, nadhani Urusi, sasa, itakabiliwa na mashambulizi makali kufuatia shambulio hili. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.