Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi nchini Urusi: Siku ya pili ya kupiga kura, kiwango rasmi cha ushiriki kiko juu

Siku ya pili ya kupiga kura kwa uchaguzi wa urais bila mashaka mengi nchini Urusi. Kwa mara ya kwanza, kura inapigwa kwa siku tatu. Vladimir Putin, aliye madarakani kwa miaka 24, alipiga kura siku ya Ijumaa Machi 15 kwenye mtandao. Ana uhakika wa kushinda uchaguzi huu ambapo atakabiliana na wagombea watatu wasiojulikana kwa umma. Uchaguzi usio na mashaka mengi, lakini kiwango cha ushiriki rasmi tayari kinaripotiwa kuwa juu.

Moja wa wapiga kura akiondoka kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa siku ya pili ya uchaguzi wa urais wa Urusi mnamo Machi 16, 2024 huko Rybezhno, huko Leningrad.
Moja wa wapiga kura akiondoka kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa siku ya pili ya uchaguzi wa urais wa Urusi mnamo Machi 16, 2024 huko Rybezhno, huko Leningrad. © Anton Vaganov / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kufikia Ijumaa, mmoja kati ya wapiga kura watatu alikuwa tayari amepiga kura, kulingana na takwimu za Tume Kuu ya Uchaguzi ya Urusi. Katika majimbo manane, kiwango cha ushiriki kimezidi 50%, au hata 60% kama katika Kemerovo, jimbo la kusini mwa Siberia. Jimbo jili lina sifa thabiti ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi.

Kama gazeti la Novaya Gazeta linavyobainisha, katika maeneo mengi ambayo yana hamu kubwa ya kupiga kura, Vladimir Putin alishinda alama za juu zaidi katika uchaguzi wa urais wa mwaka 012 na 2018.

Shirika huru la ufuatiliaji wa uchaguzi la Golos, lililopewa jina la "afisa wa kigeni", linabainisha kutokuwepo kwa waangalizi wa upinzani katika vituo vya kupigia kura na linasema kuwa katika maeneo mengi, watumishi wa umma na wafanyakazi wa makampuni makubwa, ambayo kwa kiasi fulani yanamilikiwa na serikali, wamekabiliwa na shinikizo la kupiga kura.

Hii inathibitishwa na vyombo vya habari vya mtandaoni vinavyozungumza Kirusi Agentstvo, pia huainishwa kama "afisa wa kigeni", ambavyo vimepata kwenye mitandao ya kijamii zaidi ya picha 450 au video zilizorushwa na wafanyakazi wa shule, taasisi za kitamaduni au makampuni kama vile Gazprom, wakati wanaondoka katika vituo vya kupigia kura. Vyombo vya habari vinabainisha kuwa wakati wa uchaguzi wa wabune wa hivi karibuni wa mwaka 2021, ni ripoti 31 tu za aina hii zilichapishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.