Pata taarifa kuu

Urusi yazuia mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani za Ukraine

Urusi imedai kuangusha ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine katika eneo lililokaliwa la Crimea, katika mkoa wa Moscow pamoja na ile ya Belgorod na Voronezh, karibu na Ukraine.

Roketi za Urusi zinarushwa dhidi ya Ukraine kutoka eneo la Belgorod nchini Urusi, zinazoonekana kutoka Kharkiv, Ukraine, Jumapili, Julai 16, 2023.
Roketi za Urusi zinarushwa dhidi ya Ukraine kutoka eneo la Belgorod nchini Urusi, zinazoonekana kutoka Kharkiv, Ukraine, Jumapili, Julai 16, 2023. AP - Vadim Belikov
Matangazo ya kibiashara

Ndege kadhaa ziliharibiwa katika eneo lililounganishwa la Crimea, katika mkoa wa Moscow na ile ya Belgorod na Voronezh, usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu.

"Drones zilinaswa juu ya maeneo ya magharibi, kusini-magharibi, kaskazini-magharibi na mashariki mwa peninsula ya Crimea, Istra (magharibi) na Domodedovo (kusini) wilaya za mkoa wa Moscow, mikoa ya Belgorod na Voronezh (kusini-magharibi)," Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwenye Telegramu, bila kubainisha idadi ya ndege zilizoharibiwa au kuripoti uharibifu au majeruhi kufikia hatua hii.

"Vituo vya uzalishaji wa kiwanda cha kivita cha Kharkiv, ambapo ukarabati na utunzaji wa magari ya kivita ya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine ulikuw ukifanyika, vlipigwa na mashambulizi haya anga," chanzo hicho pia kimetangaza.

Moja ya makampni ya Kharkiv yalengwa na makombora

Hapo awali, mkuu wa utawala wa jeshi la Ukraine, Oleg Synegubov, aliripoti kwenye Telegram kwamba moja ya makampuni katika jiji hilo ilipigwa na "makombora manne ya S-300" na moto ukazuka.

Kharkiv na jimbo la jina moja ziko kusini mwa Belgorod nchini Urusi. Siku ya Jumapili, ulinzi wa anga wa Urusi uliidungua ndege isiyo na rubani ya Ukraine katika mkoa wa Moscow na zingine sita kuelekea peninsula ya Crimea. Aina hii ya mashambulio yaliyofanywa na Kiev dhidi ya eneo la Urusi, mji mkuu wake au Crimea iliyotwaliwa mwaka 2014 yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni katikati ya mashambulizi ya Kyiv yaliyoanza mwanzoni mwa mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.