Pata taarifa kuu

Urusi: Jenerali Surovikin, anayejulikana kuwa karibu na Wagner, aonekana tena

'Jenerali Armaggedon' alikuwa alikuwa ahaonekani hadharani tangu kundi la mamluki la Wagner kuasi mwishoni mwa mwezi Juni. Wakati huu, picha zake kadhaa huko Algeria na ujumbe kutoka Wizara ya Ulinzi ziliwekwa wazi kwenye vyombo vya habari vya Urusi. Mustakabali wa Sergei Surovikin bado uko mashakani.

Jenerali wa Urusi Sergei Surovikin, wakati huo akiwa kamanda wa Kundi la pamoja la majeshi ya Urusi nchini Ukraine, Oktoba 18, 2022.
Jenerali wa Urusi Sergei Surovikin, wakati huo akiwa kamanda wa Kundi la pamoja la majeshi ya Urusi nchini Ukraine, Oktoba 18, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow, Anissa El Jabri

Baada ya picha ya kwanza siku kumi na mbili zilizopita - iliyochapishwa kwenye Telegram na haijathibitishwa - ikimuonyesha akienda kwenye mgahawa, bila shaka katika eneo la mji mkuu wa Urusi, wakati huu, inaonekana kwamba Sergei Surovikin yuko hai.

Picha kadhaa zinazomuonyesha zilichapishwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano kwenye ukurasa wa Facebook wa msikiti mmoja huko Oran. Imebainishwa kwamba “ujumbe wa ngazi za juu wa Urusi” ulipokelewa na mkurugenzi wa mambo ya kidini na wakfu pamoja na na imamu. Jenerali Sourovikin anaonekana katika ujumbe huo akivalia sare inayofanana na mchanga, bila alama yoyote inayoonyesha cheo chake na bila medali. Tangu mwanzoni mwa mwezi Septemba, wasifu wake pia umetoweka kutoka kwa wavuti ya Wizara ya Ulinzi. Vyombo vya habari kadhaa vya Urusi hapo awali viliripoti kujiuzulu kwake kama kamanda wa vikosi vya anga.

Maoni yasiyojulikana

Ilichukua siku mbili kwa picha hizi kuonekana nchini Urusi kwenye vituo kadhaa vya habari vya Telegraph, ambavyo vingine vinajulikana kuwa karibu na kundi la Wagner, lakini pia kwenye vyombo vya habari, wakati huu na maoni ambayo hayakujulikana lakini kutoka kwa vyanzo vya jeshi.

Kwa nini Jenerali Surovikin anatokea tena hivi, zaidi ya wiki tatu baada ya kuanguka kwa ndege iliyombeba Yevgeny Prigozhin na waandamizi wake kadhaa, akiwemo Dimitri Outkin.

Kwa mujibu wa moja ya vyanzo vya kijeshi vilivyotajwa na gazeti la Kommersant, "ni dhahiri kwamba Surovikin anaendelea kuaminika kwa kiwango cha juu na inawezekana kwamba safari ya jenerali inahusishwa na uteuzi unaowezekana wa baadaye."

Chanzo kingine kilichonukuliwa wakati huu na Gazeti la kila siku la Les Izvestia kinabainisha kuwa "hii sio ziara ya kijeshi, lakini mkutano wa kiserikali ambao mifumo ya silaha inapendekezwa." Sourovikin alikuwepo tu kama "mgeni wa heshima".

Kituo cha Telegraph cha VCHK-OGPU kinabainisha kwamba, "licha ya hadhi rasmi ya hafla hiyo, Surovikin alivaa nguo za kiraia kwenye mikutano yote, ambayo inathibitisha kufukuzwa kwake kutoka kwa jeshi la Urusi." Idhaa hiyo inadokeza kuwa kiuhalisia utawala wa rais ndio uliweza kupata idhini kwa jenerali huyo kushiriki katika hafla. Kwa mujibu wa VCHK-OGPU, "hii inashuhudia kuanza kwa kampeni inayolenga kuchukua nafasi ya Prigozhin na sura ya Surovikin, kwenye soko la ndani na la kimataifa, ili kuwa na nguvu inayokua ya Shoigu ndani ya mamlaka. "

Tangu uasi mwishoni mwa mwezi Juni, picha ambazo zimevuja katika safari ndani ya nchi ambako Wagner ilishiriki zilionyesha tu maafisa wa ngazi ya juu wa Urusi, akiwemo Naibu Waziri wa Ulinzi Yunus Bek-Yevkourov.

Alipanga ujenzi wa mistari ya ulinzi

Sergei Surovikin aliteuliwa kuwa kamanda wa Kundi la Pamoja la Vikosi vya Urusi huko Ukraine mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2022. Ni yeye ambaye alichukua jukumu la uondoaji wa jeshi kutoka mji wa Kherson na kuandaa ujenzi wa mistari ya ulinzi. Mnamo Januari 11, 2023, rais wa Urusi Vladimir Putin alimfukuza na nafasi yake ikachukuliwa na Valery Gerasimov, Mkuu wa majeshi.

Jenerali Surovikin ambaye aliteuliwa mnamo Mei 2023 na Yevgeny Prigozhin kama mpatanishi kati ya jeshi na yeye juu ya suala la usambazaji wa silaha na risasi, alionekana kwa mara ya mwisho mbele ya umma wa Urusi usiku wa uasi mnamo Juni 23. Akiwa na bunduki kwenye magoti yake, aliwaomba wapiganaji wa Wagner kwenye video wasimame. Vyombo kadhaa vya habari tangu wakati huo vinadai kwamba alishutumiwa kuwa alikuwa anajua maandalizi ya uasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.