Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Jeshi la Urusi ladai kuzima mashambulio ya ndege zisizo na rubani za Ukraine

Urusi imedai kuharibu ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine katika maeneo ya mpakani ya Bryansk na Belgorod (magharibi) usiku wa Jumatano Septemba 13 kuamkia Alhamisi Septemba 14, bila kuripoti majeruhi yoyote katika hatua hii.

Makombora matatu ya Urusi yayorushwa dhidi ya Ukraine kutoka jimbo la Belgorod nchini Urusi yanaonekana alfajiri huko Kharkiv, Ukraine, Alhamisi, Machi 9, 2023.
Makombora matatu ya Urusi yayorushwa dhidi ya Ukraine kutoka jimbo la Belgorod nchini Urusi yanaonekana alfajiri huko Kharkiv, Ukraine, Alhamisi, Machi 9, 2023. AP - Vadim Belikov
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya jeshi la Urusi vimedungua ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine katika maeneo ya Bryansk na Belgorod bila kusababisha hasara yoyote.

Katika taarifa nne tofauti, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imebaini kwenye Telegram kwamba ndege sita zisizo na rubani zilidunguliwa kati ya saa nne usiku Jumatano (saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati) na saa sita na dakika 45 usiku (sawa na saa tano na dakika 45 usiku saa za Afrika ya Kati) katika eneo la mkoa wa magharibi wa Bryansk, unaopakana na Ukraine.

Gavana wa mkoa huo Alexander Bogomaz pia ameripoti kwenye Telegram idadi ya ndege sita zilizoharibiwa kwenye anga ya wilaya za Ounetchski, Brasovski, Starodubski na Karatchevksi, wilaya iliyo karibu na jiji la Briansk. Hakukuwa na waathiriwa au uharibifu, kulingana na Alexandre Bogomaz.

Mashambulio mengi ya ndege zisizo na rubani katika wiki za hivi karibuni

Hapo awali, Ulinzi wa Urusi uliripoti kwamba ndege nyingine isiyo na rubani ya Ukraine ilidunguliwa saa tatu na dakika 30 usiku kwa saa za huko siku ya Jumatano (saa mbili na dakika 30 usiku Afrika ya Kati) kwenye jimbo la Belgorod, linalopakana na jimbo la Ukraine la Kharkiv kusini zaidi. Gavana Vyacheslav Gladkov amesema kuwa kifaa hicho kilinaswa juu ya kijiji cha Toulyanka, kilomita chache kutoka Ukraine.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine dhidi ya maeneo ya Urusi, iwe mikoa ya karibu na Ukraine, iliyotwaa Crimea au mji mkuu Moscow, yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni katikati mwa majibu ya mashambulizi ya Kiev yaliyoanza mwanzoni mwa mwezi Juni.

Urusi ilisema kuwa iliharibu ndege mbili za anga za Ukraine siku ya Jumatatu katika jimbo la Belgorod, kisha magari matatu ya wanamaji siku ya Jumatano katika Bahari Nyeusi baada ya shambulio la kwanza asubuhi dhidi ya kituo cha meli cha Urusi huko Sevastopol, katika eneo lililotekwa la Crimea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.