Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Wawili wawauawa baada ya shambulio la kombora katika mji wa Kyiv

"Shambulio la kombora" limelenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv Jumatano asubuhi, ambapo milipuko imesikika, mamlaka ya kiraia na kijeshi ya Ukraine imeripoti. Kulingana na meya wa jiji hilo, Vitali Klitschko, takriban watu wawili wamefariki na mwingine mmoja kujeruhiwa.

Mji wa Kyiv umelengwa na kombora liloua watu wawili na kujeruji mwengine mmoja.
Mji wa Kyiv umelengwa na kombora liloua watu wawili na kujeruji mwengine mmoja. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

"Kwa bahati mbaya, kufuatia kuanguka kwa mabaki ya kombora katika wilaya ya Shevchenkivskyi ya Kiev (...) watu wawili wamefariki, kulingana na taarifa za awali. Mtu mwingine amejeruhiwa," Mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji mkuu wa Ukraine, Sergey Popko, amesema kwenye Telegram.

"Ni kweli kumetokea shambulio la kombora. Katika wilaya ya Darnytskyi ya Kiev, mabaki ya kombora yameanguka juu ya paa la jengo la kibiashara. Idara ya huduma za dharura zilikwenda kwenye eneo la tukio," amesema dakika chache mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.