Ukraine: Marubani watatu wa kivita wafariki baada ya ndege kugongana
Nchini Ukraine, marubani watatu walifariki wakati wa mafunzo siku ya Ijumaa. Pigo jipya kwa Kyiv, wakati nchi hiyo inaadhimisha Siku maksusi ya usafiri wa anga Jumapili hii, Agosti 27.
Imechapishwa:
Na mwandishi wetu huko kyiv, Emmanuelle Chaze
Katika mkoa wa Zhytomyr, magharibi mwa Kiev, Jeshi la Anga limethibitisha vifo vya marubani wake watatu, waliofarikisik ya Ijumaa Agosti 25 baada ya ndege za mafunzo za L-39 kugongana angani.
Mamlaka imetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi kubaini sababu za mkasa huo uliotokea siku ya Ijumaa. Miongoni mwa wahanga rubani wa kivita aliyepewa jina la "Juice", ambaye alifanya mashambulizi kadhaa ndani ya gari lake aina ya Mig-29 kuhami, miongoni mwa mambo mengine, mji mkuu wa Kiev.
Kuwafunza marubani wake kwenye ndege aina ya F-16
Vifo vya marubani hawa watatu ni pigo kwa Ukraine, ambayo inakuja katika wakati muhimu ambapo nchi iko katika mbio dhidi ya wakati kwa kutoa mafunzo, nchini Ukraine na nje ya nchi, vipengele vyake bora katika uongozaji wa ndege maarufu ya kivita ya F-16 iliyoahidiwa na washirika wake wa Magharibi. Serikali tayari imeonya kwamba ndege hizi zitawasilishwa mara tu marubani wake watakapofahamu matumizi yao, kwa upande wa Kyiv hii inamaanisha kuwa F16 hazitakuwa Ukraine hadi mapema 2024.
Aidha, watu wawili waliuawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulio la bomu la Urusi katika kijiji cha Podoly cha Ukraine, karibu na mji wa Kupiansk, kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, alitangaza gavana wa eneo hilo Jumamosi Agosti 26.