Pata taarifa kuu

Moscow inasema imezima shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine

Urusi inasema imezima shambulio jipya la ndege zisizo na rubani jijini Moscow, meya wa jiji hilo amesema. Hili ni jaribio la hivi punde kati ya majaribio kadhaa ya kushambulia mji mkuu wa Urusi kwa ndege zisizo na rubani wiki hii.

Muonekano unaonyesha sehemu iliyoharibiwa  ya jengo la ghorofa ya juu katika Jiji la Moscow kufuatia shambulio linalodaiwa kuwa la ndege zisizo na rubani za Ukraine mjini Moscow, Urusi, Agosti 23, 2023. REUTERS/Stringer
Muonekano unaonyesha sehemu iliyoharibiwa ya jengo la ghorofa ya juu katika Jiji la Moscow kufuatia shambulio linalodaiwa kuwa la ndege zisizo na rubani za Ukraine mjini Moscow, Urusi, Agosti 23, 2023. REUTERS/Stringer RUSSIA - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Meya wa Moscow Sergei Sobyanin, mapema leo Jumamosi ameeleza kwamba ndege isiyo na rubani iliharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga katika wilaya ya Istra magharibi mwa Moscow.

Huduma za dharura zilikuwa zimesitishwa kwenye eneo la tukio na hakujawa na ripoti za awali za uharibifu au majeruhi kwa mujibu wa Meya huyo.

Shambulio la ndege zisizo na rubani siku ya Jumamosi lilipelekea mamlaka kwenye eneo husika kufunga kwa muda viwanja vyote vitatu vya ndege vinavyohudumia mji mkuu.

Jeshi la Urusi limeripoti kuwa ndege zisizo na rubani za Ukraine na shambulio la kombora katika baadhi ya maeneo nchini humo katika kipindi cha wiki moja iliyopita, na viwanja vya ndege vitatu vya Moscow - Sheremetyevo, Domodedovo na Vnukovo, vimelazimika kusimamisha safari za ndege kwa muda kutokana matukio hayo.

Safari za ndege pia zilitatizwa katika viwanja vya ndege vya Moscow siku ya Jumanne, Jumatano na Ijumaa, kulingana na ripoti.

Ukraine haikutoa maelezo  yake mara moja kuhusu uvamizi wa hivi punde wa ndege zisizo na rubani na imekuwa ikikana hadharani kuhusika na mashambulio ndani ya Urusi au katika eneo linalodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliripoti siku ya Ijumaa kwamba vikosi vyake vilidungua ndege tisa za Ukraine zisizo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.