Pata taarifa kuu

Uturuki yatarajia kufufua mpango wa nafaka wa Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anatarajiwa nchini Ukraine siku ya Ijumaa tarehe 25 Agosti. Mazungumzo yake yatazingatia mpango wa uuzaji wa nafaka wa Ukraine, ambao Urusi iilijiondoa Julai 17. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan bado ana matumaini ya kumshawishi mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kurejea katika makubaliano hayo. Baada ya Ukraine, Hakan Fidan pia anaweza kwenda Urusi katika siku zijazo.

Urusi ilijiondoa katika makubaliano ya mauzo ya nafaka ya UkrainE mnamo Julai 17, 2023.
Urusi ilijiondoa katika makubaliano ya mauzo ya nafaka ya UkrainE mnamo Julai 17, 2023. Danil SEMYONOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Istanbul, Anne Andlauer

Uturuki inaongeza juhudi zake za kufufua makubaliano ya korido za nafaka kabla ya mavuno ya msimu huu. Hofu ni ile ya kupanda upya kwa bei za vyakula duniani, lakini pia kuongezeka kwa mvutano katika Bahari Nyeusi, wakati ambapo Ukraine inataka kuuza bidhaa zake za kilimo kwa njia ya bahari bila kupitia makubaliano na Urusi.

Mnamo Agosti 17, meli ya mizigo iliyokuwa ikitoka Ukraine ilifika Istanbul licha ya vikwazo vya Urusi, ikipitia kile rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliita "ukanda mpya wa kibinadamu". Wakati akielewa hitaji la Kyiv kuuza nafaka yake, Uturuki ina wasiwasi kuhusu mipango hii. Shambulio la Urusi dhidi ya meli zinazoondoka au kuelekea bandari za Ukraine bado linawezekana. Hii inafanya njia hizi mbadala kuwa hatari sana, na kwa hivyo kuwa za gharama kubwa katika suala la bima, na athari inayowezekana ya kuongezeka kwa bei ya nafaka.

Uturuki inapendelea mazungumzo na kutafuta suluhu litakalokidhi matakwa ya Urusi, yaani, kuondolewa kwa vikwazo kwa mauzo yake ya nje ya bidhaa za kilimo. Recep Tayyip Erdogan na Vladimir Putin wanaweza kukutana katika wiki zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.