Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Mwandishi wa habari wa Urusi kutoka shirika la habari la Ria Novosti auawa

Mwanahabari wa Urusi kutoka shirika la habari la Ria Novosti, Rostislav Jouravlev, ameuawa katika shambulizi la anga la Ukraine katika eneo la Zaporizhia kusini mwa Ukraine siku ya Jumamosi. taarifa hii ya mauaji haya yametolewa na jeshi la Urusi katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Rostislav Jouravlev, mwandishi wa masuala ya vita wa shirika la habari la Urusi Ria Novosti, aliuawa Jumamosi Julai 22 nchini Ukraine. Picha isiyo na tarehe iliyochapishwa na shirika la habari la Sputnik.
Rostislav Jouravlev, mwandishi wa masuala ya vita wa shirika la habari la Urusi Ria Novosti, aliuawa Jumamosi Julai 22 nchini Ukraine. Picha isiyo na tarehe iliyochapishwa na shirika la habari la Sputnik. AP
Matangazo ya kibiashara

Rostislav Jouravlev alikuwa mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ria Novosti. "Vitengo vya wanajeshi wa Ukraine vilianzisha shambulio la mizinga dhidi ya kundi la waandishi wa habari […] na kuwajeruhi waandishi wa habari wanne zaidi au kidogo," jeshi la Urusi limesema. Wakati wa akisafirishwa hospitalini, Rostislav Jouravlev amefariki kutokana na majeraha yake kufuatia mlipuko wa bomu”. Hali ya wanahabari wengine watatu waliojeruhiwa "iko sawa". Jeshi la Urusi limesema kwamba "wamesafirishwa haraka hadi kwenye vituo vya matibabu" vya Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Kulingana na mwajiri wa Rostislav Jouravlev, shirika la habari la Ria Novosti, "mashambulizi ya makombora yamefanyika karibu na kijiji cha Pyatikhatky", katika eneo la Zaporizhia. Gavana wa mkoa aliyewekwa na Moscow, Yevgeny Balitsky, amethibitisha kifo cha mwandishi wa habari kwenye Telegram, akitoa "rambirambi [zake] za kina kwa familia na marafiki".

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imeelezea kifo cha kukusudia katika shambulio la anga la Ukraine kwa mwandishi wa habari wa Urusi kama "uhalifu mbaya", ikishtumu nchi za Magharibi "zinazoisadia" Kiev na kuahidi "jibu" kwa wale waliohusika na shambulio hili. "Kila kitu kinaonyesha kuwa shambulio dhidi ya kundi la waandishi wa habari halikufanywa kwa bahati mbaya," diplomasia ya Urusi imesema katika taarifa. "Tuko sahihi kwamba mashirika ya kimataifa yenye uwezo yatapendelea, kama hapo awali katika kesi kama hizo, kufumbia macho uhalifu huu wa kutisha. "

Mpiga picha wa Ujerumani wa Deutsche Welle ajeruhiwa

Wakati huo huo, mpiga picha wa Ukraine, Ievguen Chylko, akipiga picha na timu ya Deutsche Welle, kilomita 23 kutoka uwanja wa vita upande wa Ukraine, amejeruhiwa "na mlipuko wa bomu la Urusi", imebainisha kituo kimoja cha televisheni. Wakati wa tukio hili, mwanajeshi wa Ukraine aliuawa "na wengine walijeruhiwa vibaya", kituo hiki cha televisheni kimeongeza katika taarifa.

Wanahabari wengine wawili wa timu ya idhaa hiyo, mwanahabari na mshauri wa masuala ya usalama, wahajeruhiwa. Walikuwa walikuwa wakirekodi kipindi kuhusu kituo cha mafunzo cha jeshi la Ukraine "karibu na Druzhkivka" huko Donbass, Mkoa wa Donesk. "Lengo la shambulio la Urusi labda lilitekelezwa dhidi ya uwanja wa mazoezi wa Ukraine," Deutsche Welle alisema.

Wakati huo huo, kituo cha televisheni ya umma ya Ujerumani Deutsche Welle imeripoti kwamba mmoja wa wapiga picha wake kutoka Ukraine amejeruhiwa na mabomu ya kivita ya Urusi alipokuwa akiripoti kuhusu jeshi la Ukraine karibu na uwanja wa vita.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.