Pata taarifa kuu

Urusi: Mwanablogu mwenye ushawishi Igor 'Strelkov' Girkin akamatwa kwa itikadi kali

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa nchi inayojiita Jamhuri ya Donetsk alikamatwa Ijumaa Julai 21 huko Moscow. Nyumba ya Igor Girkin, inayojulikana kwa jina la bandia la "Strelkov", pia ilifanyiwa ukaguzi. Ukosoaji wa mara kwa mara wa uongozi wa jeshi la Urusi kutoka kwa mwanablogu huyu mwenye msimamo mkali bila shaka umeishia kuichosha mamlaka: pengine angefunguliwa mashitaka ya itikadi kali, kulingana na wakili wake.

Mwanablogu mwenye ushawishi mkubwa Igor "Strelkov" Girkin, katika mkutano na waandishi wa habari wa kundi la wazalendo linachojulikana kama "Angry Patriots Club" huko Moscow mnamo Mei 12, 2023.
Mwanablogu mwenye ushawishi mkubwa Igor "Strelkov" Girkin, katika mkutano na waandishi wa habari wa kundi la wazalendo linachojulikana kama "Angry Patriots Club" huko Moscow mnamo Mei 12, 2023. REUTERS - MAXIM SHEMETOV
Matangazo ya kibiashara

"Alikamatwa na polisi" asubuhi, amesema wakili wake Alexander Molokhov, akiongeza kuwa "pengine" alishutumiwa kwa itikadi kali.

Mwezi Aprili mwakahuu, Igor Girkin alichunguzwa kwa kudharau jeshi la Urusi. Tangu kuanza kwa mashambulio ya Urusi, kanali huyu wa zamani wa kikosi cha FSB alikosoa vikali mwenendo wa operesheni nchini Ukraine, na kuonyesha uzembe wa makao makuu ya jeshi au Waziri wa Ulinzi wa Urusi, au hata makosa yao ya kimbinu. Na hata kuandika kwenye akaunti yake ya Telegram, inayotwa na zaidi ya watu 875,000.

Pia alitangaza mwanzoni mwa mwaka huu kwamba aliingia kwenye siasa, hivyo kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi. Moja ya ujumbe wake wa mwisho, uliochapishwa siku ya Jumanne, ulionekana kumshambulia, bila kumtaja, Rais wa Urusi Vladimir Putin. Igor Guirkin alidai kwamba "mtu mchafu" amekuwa madarakani kwa miaka 23 nchini Urusi na kwamba nchi hiyo haitaunga mkono "miaka sita zaidi ya msaliti huyu aliye madarakani".

Ukosoaji huu ulivumiliwa mara moja, lakini ni wazi kuwa sio hivyo tena leo: yule anayeitwa "Strelkov" ("mpiga risasi", kwa Kirusi) ameshutumiwa kwa msimamo mkali kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa dhidi yake na mwanachama wa zamani wa wanamgambo wa Wagner, ambapo maelezo yake hayajatangazwa.

Kwenye Telegram, mwanasayansi wa siasa Tatiana Stanovaya amebaini kwamba Igor Girkin "zamani" alivuka "mistari yote nyekundu" katika ukosoaji wake dhidi ya Kremlin na jeshi la Urusi.

Jaribio la kukandamiza wakosoaji wa mwisho, hata wazalendo

Lakini kukamatwa huku kunazua idadi fulani ya maswali nchini Urusi, na hasa yale ya uhusiano unaowezekana na asili yake kati ya mtu huyu mwenye msimamo mkali na wanamgambo wa Wagner. Kwa hivyo viongozi wameamua kupiga kipenga cha mwisho kwa mchezo wa "Strelkov".

"Kukamatwa kwake bila shaka ni kwa maslahi ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Hii ni moja ya matokeo ya uasi wa Prigozhin: jeshi limepata fursa zaidi za kukandamiza wapinzani wake katika nafasi ya umma," Tatiana Stanovaya amesema.

Ahukumiwa maisha katika kesi ya ndege MH17

Igor Girkin pia ni miongoni mwa wanaume waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama za Uholanzi kwa kudungua ndege ya shirika la ndege la Malaysian Airlines MH17 kwa kombora katika anga ya Ukraine mwaka 2014. Abiria 298 na wafanyakazi wake walifariki.

Alijipatia jina kwa muda mfupi kuwa kiongozi wa kijeshi wa waasi wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine mnamo mwaka 2014. Alitawala ngome inayotaka kujitenga ya Sloviansk kwa mkono wa chuma, lakini alitangaza kujiuzulu mnamo mwezi Agosti 2014 katika hali ya kushangaza, kabla ya kurejea Urusi ambapo alikuwa amepoteza ushawishi wowote.

(Pamoja na mashirika)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.