Pata taarifa kuu

Watu wawili wameuawa katika shambulio la Urusi kwenye mji wa Odesa

Nairobi – Wanajeshi wa Urusi kwa siku ya tatu, wameshambulia mji wenye bandari ya  Odesa na kusababisha vifo vya watu wawili na kuwajeruhi wengine 20. Majengo katika eneo hilo bandari yameharibiwa.

Watu wengine 20 wameripotiwa kujeruhiwa kwenye shambulio hilo
Watu wengine 20 wameripotiwa kujeruhiwa kwenye shambulio hilo REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema, kuanzia siku ya Ijumaa, itashambulia meli zinazokwenda katika bandari za Urusi na ile Nyeusi, katika eneo linalodhibitiwa na vikosi vya Moscow na kuamini kuwa  vinabeba silaha za kivita.

Umoja wa Mataifa umesema utaongeza muda wa wa vikwazo dhidi ya Urusi kwa miezi sita zaidi, kuizuia kusafirisha nafaka zake kwenye soko la Kimataifa.

Tangazo hili limekuja baada ya wiki hii, Urusi kujiondoa kwenye mkataba na Ukraine, uliokuwa unaruhusu Kiev kusafirisha nafaka zake kupitia bahari nyeusi.

Aidha, EU kupitia mkuu wake wa sera za kigeni Josep Borrell, imesema Umoja huo utatoa Euro Milioni 20 kuisaidia Ukraine kuishinda Urusi kwenye vita vinavyoendelea.

Urusi nayo imetangaza kuwa wanadiplomasia wa Uingereza wanaofanya kazi nchini humo, watalazimika kutoa taarifa kwa mamlaka, kuhusu ziara zao katika ardhi ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.