Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Urusi Odessa: UNESCO 'inaalaani vikali' shambulio dhidi ya urithi wa ulimwengu

UNESCO siku ya Ijumaa "ilishutumu vikali" mashambulizi ya Urusi yaliyofanywa "mapema Alhamisi asubuhi" dhidi ya eneo la katikati mwa jiji la Odessa (kusini-magharibi mwa Ukraine), ambalo ni sehemu ya urithi wa dunia tangu mwezi Januari.

Mji wa Odessa Ulikumbwa hivi karibuni na mashambulizi ya anga ya Urusi.
Mji wa Odessa Ulikumbwa hivi karibuni na mashambulizi ya anga ya Urusi. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na tathmini ya awali, makumbusho kadhaa yaliyo ndani ya eneo la Urithi wa Dunia yalikumbwa na uharibifu, ikiwa ni pamoja na Makumbusho ya Akiolojia, Makumbusho ya Fleet na Makumbusho ya Fasihi ya Odessa," shirika la Umoja wa Mataifa la utamaduni, sayansi na elimu limesema.

"Zote zilikuwa zimetiwa alama na UNESCO na mamlaka za ndani na Ngao ya Bluu, nembo ya kipekee ya Mkataba wa Hague wa 1954" kwa ajili ya ulinzi wa mali ya kitamaduni katika tukio la vita vya silaha, ambayo kwa hiyo "ilikiukwa" huko Odessa, imeshutumu UNESCO.

Mali ya kitamaduni iliyolindwa kushambuliwa

Shambulio la Urusi, "lililofanywa wiki mbili tu baada ya lile lililoharibu jengo" katika kituo cha kihistoria cha Lviv (Kaskazini-Magharibi), eneo lingine la urithi wa ulimwengu, pia "liliendana na uharibifu wa Kituo cha Utamaduni cha Sanaa ya Watu na Elimu ya Sanaa katika jiji la Mykolaiv", UNESCO imebainisha.

Shirika hili la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa "kukomesha mashambulizi yote dhidi ya mali ya kitamaduni inayolindwa ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa zilizoidhinishwa".

"Vita hivi vinaleta tishio linaloongezeka kwa utamaduni wa Ukraine," UNESCO imesema, ikiongeza kwamba imerekodi "uharibifu kwa maeneo 270 ya kitamaduni nchini Ukraine" tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, 2022.

Kituo cha kihistoria cha Odessa, jiji maarufu kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi, kiliandikwa mnamo Januari 2023 kwenye orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia katika hatari kutokana na "vitisho vya uharibifu" vinavyozunguka kutokana na vita kwenye eneo hili, hatari zaidi kwa kuwa liiko karibu na bandari, miundombinu ya kimkakati kwa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.