Pata taarifa kuu

Covid-19: Australia kufungua tena mipaka yake

Wakati zaidi ya 85% ya wakazi wa Australia walio na umri wa zaidi ya miaka 16 sasa wakipatiwa chanjo, Canberra imeamua kufungua tena mipaka ya nchi hiyo. Waziri Mkuu ametangaza hivi punde kwamba watu walio pewa chanjo, wanaweza kuingia nchini Australia kuanzia mwezi ujao.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrisson Novemba 22, 2021 huko Canberra.
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrisson Novemba 22, 2021 huko Canberra. © Lukas Coch/AAP Image via AP
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi chote cha janga, Australia ilijitofautisha na nchi zingine kwa kuchukuwa hatua kadhaa dhidi ya COVID-19, hususan kufunga mipaka yake kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Baada ya kuruhusu raia wa Australia au wakaazi wa nchi hiyo waliopewa chanjo kurudi nchini bila kuwekwa karantini mwanzoni mwa mwezi huu, Scott Morrison ametangaza ufunguzi kamili wa mipaka ya nchi yake kwa wageni, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Canberra.

"Kuanzia Desemba 1, 2021, abiri wenye viza wanaostahiki ambao wamechanjwa mara mbili wataweza kuja Australia," amesema. Aina za visa zinazostahiki ni pamoja na viza kwa makundi ya wafanyakazi wenye ujuzi na wanafunzi, lakini pia visa vinavyotolewa kwa watu wanaohudumu katika mashirika ya kutoa misaada, visa ya kufanya kazi ya likizo.

Motisha za kiuchumi

Lengo pia ni kusaidia ufufuaji wa uchumi, anaripoti mwandishi wetu wa Sydney, Grégory Plesse. Wanafunzi wa kigeni, kwa mfano, kawaida huchangia euro bilioni 25 kwa mwaka. Lakini pia kushughulikia haraka iwezekanavyo uhaba wa wafanyakazi unaokabili uchumi wa Australia. Ndiyo maana Karen Andrews, Waziri wa Mambo ya Ndani, ana shauku ya kuona wahamiaji laki kadhaa wakiwasili katika miezi ijayo.

"Makadirio yetu ni kwamba watu 200,000 watakuja katika miezi michache ijayo. Takwimu hii inaweza kuzidi. Kilicho hakika ni kwamba tutakuwa tukifanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kwamba watu wengi wanafika Australia haraka iwezekanavyo, "amebaini.

Ni lazima kusema kwamba uhaba huu wa kazi unaathiri sekta zote za uchumi. Kulingana na takwimu za hivi majuzi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Australia, nafasi zimesalia wazi katika 20% ya kampuni katika sekta zote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.