Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Australia yafunga mpaka kati ya majimbo yake mawili yenye wakazi wengi

Serikali ya Australia kwa mara ya kwanza katika miaka 100 imetangaza itafunga  mipaka yake jimbo la  New South Wales  na Victoria kuanzia Jumanne wiki hii kwa muda usiojulikana, katika mkakati wa kudhibiti kusambaa ugonjwa wa Corona ambao umeambukiza zaidi ya watu 8,500.

Waziri mkuu wa  Jimbo la Victoria Daniel Andrews amebaini kuwa hatua hii inajiri baada ya kuripotiwa visa 127 ndani ya siku moja, huku idadi ya vifo ikiongezeka hadi 105.
Waziri mkuu wa Jimbo la Victoria Daniel Andrews amebaini kuwa hatua hii inajiri baada ya kuripotiwa visa 127 ndani ya siku moja, huku idadi ya vifo ikiongezeka hadi 105. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Australia itafunga mpaka kati ya majimbo yake mawili yenye wakazi wengi kuanzia Jumanne wiki hii na hii kwa kipindi kisichojulikana ili kudhibiti janga la Corona ambalo linaendelea mki mkuu wa Jimbo la Victoria, Melbourne, " amesema Waziri mkuu wa  jimbo la Victoria Daniel Andrews.

Daniel Andrews amebaini kuwa hatua hii inajiri baada ya kuripotiwa visa 127 ndani ya siku moja, huku idadi ya vifo ikiongezeka hadi 105.

Mipaka ya jimbo la New South Wales na Victoria ulifungwa kwa mara ya mwisho mnamo mwaka 1919 wakati wa janga la homa iliyoanzia nchini Uhispania.

Idadi ya visa vya maambukizi huko Melbourne, mji mkuu wa jimbo la Victoria, iliongezeka katika siku za hivi karibuni, na kulazimu mamlaka ya mji huo kuweka masharti ya kutokaribianana na kuchukua hatua ya raia kutotembea katika eneo la Kaskazini lenye wakazi 300,000.

Hatua hiyo inatarajiwa kuathiri uchumi wa Australia, ambao unaelekea kuporomoka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka karibu 30. Mpaka mwingine wa jimbo la Victoria, na jimbo la Australia Kusini, tayari umefungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.