Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Jimbo la Victoria kuanza kulegeza masharti

Jimbo la Australia la Victoria linatarajia kuanza kuondoa marufuku ya raia kutotembea Jumatano baada ya kesi mbili tu mpya za COVID-19 kuripoitiwa leo Jumanne, Waziri Mkuu wa Jimbo hilo Daniel Andrews amesema.

Afisa wa afya akimhudumia mtu aliyekuja kupima corona
Afisa wa afya akimhudumia mtu aliyekuja kupima corona REUTERS/Kacper Pempel
Matangazo ya kibiashara

Marufuku ya watu kutotembea kwa siku tano yalianza kutumika siku ya Ijumaa katika jimbo hilo, la pili kwa idadi kubwa zaidi ya watu nchini, baada ya kupatikana kwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya Corona huko Melbourne.

Wakaazi zaidi ya milioni sita wa jimbo hilo walitakiwa lkubaki nyumbani isipokuwa kwa wale wanaofanya manunuzi muhimu, wafanyakazi au wahudumu w afya na kufanya mazoezi.

"Mkakati wetu unafanya kazi," Daniel Andrews amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

"Tuko katika nafasi nzuri ya kufanya mabadiliko kuanzia kesho usiku. Kama nilivyosema jana, siwezi kutoa ahadi thabiti kwa sababu saa ishirini na nne zijazo zitakuwa muhimu," ameongeza.

Australia imerekodi visa 29,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 909 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Kampeni ya chanjo nchini Australia itaanza Februari 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.