Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-PKK-USALAMA

Uturuki: Erdogan katika eneo la mashambulizi Ankara

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amejifikia mwenyewe Jumatano wiki hii katika eneo la mashambulizi jijini Ankara, siku nne baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyogharimu maisha ya watu 97, vyombo vya habari vya Uturuki vimearifu.

Miili ya watu waliouawa ikifunikwa na mabango na bendera Oktoba 10, 2015 jijini Ankara baada shambulio baya zaidi katika historia ya Uturuki.
Miili ya watu waliouawa ikifunikwa na mabango na bendera Oktoba 10, 2015 jijini Ankara baada shambulio baya zaidi katika historia ya Uturuki. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Recep Tayyip Erdogan licha ya kukusolewa vikali baada ya mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya watu wengi katika historia ya nchi ya Uturuki, amweka shada la maua katika kituo kikuu cha magari jijini Ankara, kulikotokea mashambulizi. Rais Recep Tayyip Erdogan ameambatana na mwenzake wa Finland, Sauli Niiniston, ambaye yuko ziarani Uturuki.

Jumamosi asubuhi, milipuko miwili imepiga karibu na kituo kikuu cha magari jijini Ankara, ambapo maelfu ya wanaharakati kutoka nchini kote Uturuki walikua wameitikia wito wa vyama vingi vya wafanyakaz , mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya mrengo wa kushoto vinavyounga mkono msimamo wa Wakurdi walioandamana kwa kukemea kuanza kwa mgogoro wa Kikurdi.

Awali serikali ilibaini kwamba mashambulizi mawili yaliyolenga maandamano ya amani Jumamosi mjini Ankara, nchini Uturuki, na kusababisha vifo vya watu 97, yalitekelezwa na watu wawili waliojitoa mhanga, Waziri mkuu wa Uturuki.

" Kuna ushahidi wa kutosha kwamba shambulio hilo limetekemezwa na watu wawili waliojitoa mhanga ", Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.