Pata taarifa kuu
WIKILEAKS-UFARANSA-MAREKANI-UDUKUZI

WikiLeaks : NSA yadukua simu za Chirac, Sarkozy na Hollande

Kulingana na nyaraka za WikiLeaks ziliyonukuliwa na magazeti ya kila siku ya Libération na Mediapart Jumanne Juni 23, zimu za Jacques Chirac, Nicolas Sarkozy na François Hollande zilisikilizwa na Idara ya ujasusi ya Marekani (NSA), angalau kati ya mwaka 2006 na 2012.

Simu za Jacques Chirac, Nicolas Sarkozy na François Hollande zilidukuliwa na Marekani.
Simu za Jacques Chirac, Nicolas Sarkozy na François Hollande zilidukuliwa na Marekani. DSK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Elysée imetangaza Jumanne jioni wiki hii. Baraza la kitaifa la ulinzi nchini Ufaransa linatazamiwa kukutana leo Jumatano saa tatu kamaili ( saa za Ufaransa).

" Moja kwa moja au kwa karibu muongo mmoja, simu za marais watatu wa Ufaransa zilikua zikisikilizwa na Idara za ujasusi za Marekani, kulingana na nyaraka za siri kutoka NSA", gazeti la kila siku la Mediapart limethibitisha, huku likionyesha maelezo ya Idara ya ujasusi ya Marekani.

Ripoti hizi tano za NSA zilikua zinahusu " jamii ya raia wa Marekani ", huku zikiwekwa katika makundi yaliyojulikana kwa jina la operesheni " Udukuzi wa Elysée ". Ripoti hizi hazikuweka wazi " siri ya taifa ", kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Libération, lakini zilionyesha " maslahi ya NSA kwa Ufaransa " na ripoti zote hizo zilihifadhiwa kama "siri ya hali ya juu".

Kama ilivyoelezwa na Mediapart, nyaraka hizi zinaeleza " upelelezi wa ndani wa Marekani kwa Ufaransa katika masuala ya kidiplomasia, sera za ndani au masuala ya uchumi wa kila aina ".

Unaweza kusoma katika nyaraka hizi, limeandika gazeti la kila siku la Libération kwamba mwaka 2008 Nicolas Sarkozy alijichukulia mwenyewe kama " mtu ambaye anaweza kutatua mgogoro wa kifedha". Nyaraka ya mwisho iliyotolewa Mei 22 mwaka 2012, inabaini mikutano ya siri kuhusu suala la Ugiriki

“ Matabaka yote ya taasisi za uongozi yalilengwa ”

Marais watatu si pekee yao waliolengwa na Idara ya ujasusi ya Marekani (NSA), kulingana na nyaraka za WikiLeaks. Kwa mujibu wa Mediapart, "matabaka yote ya ya taasisi za uongozi wa nchi [...], kwa wakati mmoja au mwingine, yalilengwa na Marekani, kama wakurugenzi wa utawala, mawaziri, washauri wa rais na mawaziri, mabalozi pamoja na wasemaji wa taasisi mbalimbali."

Orodha ya namba za mawasiliano ya maafisa wa serikali hatimaye zilitambuliwa na vyombo hivyo viwili vya habari. Miongoni mwa wale waliolengwa, ni pamoja na balozi wa zamani wa Ufaransa mjini Washington Vimot Pierre, Claude Guéant wakati alikua katibu mkuu katika Ikulu ya Elysée au Bernard Valero, msemaji wa wizara ya mambo ya nje. Bado kuna majina mengine ya watu ambao mazungumzo yao yalidukuliwa. Hata simu za ofisini za wizara mbalimbali zililengwa.

Wakati huo huo Ikulu ya Elysée imesema Jumanne jioni wiki hii kwamba Baraza la kitaifa Ulinzi litakutana Jumatano wiki hii saa tatu kamili " ili kutathmini habari iliyochapishwa na magazeti ya Liberation na Mediapart Jumanne jioni na baadaye kuchukua hatua zinazohitajika."

Mwaka 2013, udukuzi wa simu za Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, uliyofanywa na Marekani, uliwaghadhabisha raia wa Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.