Pata taarifa kuu
PAKISTAN-NATO

Serikali ya Pakistan yakanusha kuhusika kuwasaidia wapiganaji wa kundi la Taliban

Serikali ya Pakistan imeelezea kuchukizwa kwake na ripoti ya Jumuiya ya umoja wa majeshi ya nchi za kujihami NATO ambayo imewashutumu maofisa usalama wa Pakistan kwa kuhusika na kuvujisha taarifa za kiintelijensia kwa wapiganaji wa Taliban.

Waziri mkuu wa Pakistan, Yusuf Raza Gilani
Waziri mkuu wa Pakistan, Yusuf Raza Gilani REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo ya majeshi ya NATO imeongeza kuwa wamebaini kuwa wapiganaji wa Taliban wamekuwa wakipata nguvu ya kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya kigeni nchini humo kutokana na kupata taarifa za siri toka kwa maofisa usalama wa Pakistan.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imesema kuwa baada ya majeshi ya NATO kufanya mahojiano na zaidi ya wanamgambo elfu nne wa kundi la Talibana ambao inawashikilia wamedhibitisha kupitishiwa taarifa za siri toka kwa maofisa wa Pakistan.

Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan imesema kuwa imeshangazwa na ripoti hiyo wakati nchi yao imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa majeshi ya NATO na yale ya Marekani katika kufanya mashambulizi kwenye ngome za wapiganaji wa Taliban.

Ripoti hiyo inaendelea kuzua sintofahamu kuhusu uhusiano wa majeshi ya NATO na yale ya Marekani pamoja na serikali ya Pakistan kufuatia tukio la mwaka jana ambalo ndege za NATO ziliua wanajeshi 23 wa Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.