Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

Biashara: China na Marekani waanza tena mazungumzo baada ya Trump kuondoka

Wajumbe wa China na Marekani katika mazungumzo wanaingia leo Jumatano katika mji wa Shanghai kujadili kwa undani kuhusu vita vya kibiashara vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbli, licha ya Donald Trump kukosolewa dhidi ya China, akituhumiwa kurudisha nyuma ahadi zake.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin (kushoto) Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He (katikati) na Mwakilishi wa Biashara wa Maekani Robert Lighthizer (kulia) Julai 31 Shanghai, China.
Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin (kushoto) Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He (katikati) na Mwakilishi wa Biashara wa Maekani Robert Lighthizer (kulia) Julai 31 Shanghai, China. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi kabla ya mazungumzo ya faragha, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Robert Lighthizer na Waziri wa Fedha Steven Mnuchin wamesalimiana kwa kupeana mikono na Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He - mshirika wa karibu wa Rais Xi Jinping.

Huu ni mzunguko wa kumi na mbili wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani na mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya China na Marekani tangu kushindikana kwa mazungumzo ya awali miezi mitatu iliyopita.

Beijing na Washington zimekuwa zikikabiliana tangu mwaka jana katika vita vya kibiashara ambavyo vimesababisha baadhi ya vifaa kutozwa kodi kwa zaidi ya dola bilioni 360 za biashara ya kila mwaka.

Mzozo huo pia umeenea katika sekta ya kiteknolojia baada ya kampuni kubwa ya simu ya Huawei kutoka China kuwekwa na utawala wa Marekani kwenye orodha ya makampuni hatari kwa sababu za kiusalama.

Huawei, ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya binafsi China imekuwa ikihusishwa na kutumika na serikali ya China.

Marekani na baadhi ya washirika wake wamekuwa wakidai kuwa teknolojia ya Huawei inatumika na mashirika ya ulinzi ya China kuwapeleleza.

Kwa mujibu wa sheria ya China, makampuni ya nchi hiyo yanalazimika "kuisaidia serikali katika shughuli za upelelezi wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.