Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHUMI-USALAMA

Ufaransa: Hatua ya kupandisha kodi kwa mafuta yafutwa mwaka 2019

Kufuatia kuzuka kwa mgogoro uliosababishwa na waandamanji wanaopinga kuongezwa kwa kodi ya mafuta nchini Ufaransa, serikali imesema iko tayari kuachana moja kwa moja na hatua ya kupandisha kodi ya bidhaa hiyo kama hakutapatikana "ufumbuzi mzuri."

Katika kituo cha mafuta cha Issy-les-Moulineaux, Mei 31, 2017 (picha ya kumbukumbu).
Katika kituo cha mafuta cha Issy-les-Moulineaux, Mei 31, 2017 (picha ya kumbukumbu). BENJAMIN CREMEL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa, ongezeko la kodi ya mafuta imefutwa, ametangaza François de Rugy.

"Kama hatutapata ufumbuzi sahihi, hatuna dudi kuachana na hatua hiyo, " amesema Waziri Mkuu. Hatutatekeleza hatua ya" ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa Januari 1, hatua ambayo ilizua sintofahamu na kusababisha maandamano ya kila kukicha, " ameongeza Edouard Philippe.

Lakini ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa kuanza kutumika Januari 1, 2019 "imefutwa kwa mwaka 2019," amesema kwa upande wake Waziri wa Mazingira François de Rugy kwenye televisheni ya BFM TV.

Hatua hii imekuja, baada ya maandamano ya wiki mbili kupinga nyongeza hiyo na kusabisha mali na makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa Polisi.

Waziri Mkuu Edouard Philippe, amesema serikali itaendelea na mazungumzo na waandamanaji kuhusu suala hili ambalo limeleta hasira miongoni mwa wananchi wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.