Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-BIASHARA-UCHUMI

Washington yaendelea na mazungumzo na Beijing kuhusu biashara

Utawala wa Donald Trump umeongeza juhudi katika mazungumzo yake na China katika masuala ya biashara, kwa mujibu wa Mshauri Mkuu wa masuala ya uchumi katika ikulu ya White House, Larry Kudlow.

Biashara ya nyasi kati ya Umoja wa Mataifa na China, ambayo huingiza mabilioni ya dola kwa mwaka.
Biashara ya nyasi kati ya Umoja wa Mataifa na China, ambayo huingiza mabilioni ya dola kwa mwaka. Getty Images/Echo
Matangazo ya kibiashara

Larry Kudlow amebaini kwamba mwaliko kwa duru mpya ya mazungumzo ulitumwa kwa China.

Washington "ilipokea taarifa kuwa wawakilishi wa juu wa serikali ya China walikua wanataka kuendelea na mazungumzo," alisema Jumatano jioni wiki hii katika mahojiano ya televisheni na Fox Business Network.

"Waziri wa Fedha Steve Mnuchin, ambaye anaongoza ujumbe katika mazungumzo na China, alituma mwaliko," Larry Kudlow ameongeza.

Kauli hii ya viongozi wa Marekani inakuja wakati juma lililopita Donald Trump alisema yuko tayari kutoza kodi dola bilioni 267 (sawa na euro bilioni 230) ya bidhaa kutoka China ikiwa ni pamoja na dola bilioni 200 ambazo atatangaza hivi karibuni.

Rais wa Marekani tayari aliweka ushuru wa 25% kwa dola bilioni 50 za bidhaa za China, hasa kwa mashine na vifaa vya kielektroniki.

Mapema wiki hii maafisa wawili walio na taarifa rasmi kuhusu hali hiyo walitangaza kwamba Steve Mnuchin na wawakilishi kadhaa wa Marekani walituma mwaliko kwa wenzao kutoka China kushiriki kwa duru mpya ya mazungumzo, ambayo yatakuwa ni ya kwanza tangu yale yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti ambayo hayakuzaa matunda yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.