Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZi-SIASA

Waliberia wapiga kura kumchagua rais wao mpya

Wananchi wa Liberia wanapiga kura leo, kumchagua rais mpya katika duru ya pili ya Uchaguzi ambao umesubiriwa kwa muda mrefu.

Mpiga kura akipiga kura Monrovia, mji mkuu wa Liberia, Desemba 26, 2017, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Mpiga kura akipiga kura Monrovia, mji mkuu wa Liberia, Desemba 26, 2017, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Ushindani ni kati ya Makamu wa rais wa sasa Joseph Boakai na mchezaji wa zamani wa soka George Weah, aliyeibuka mshindi katika duru ya kwanza.

Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa mbili asubuhi saa za Afrika Magharibi.

Wapiga kura Milioni 2.1 wamejisajali kama wapiga kura ambao watashiriki uchaguzi huo.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi George Weah, mwenye umri wa miaka 51 alishinda kwa 38% ya kura na Joseph Boakai, mwenye umri wa miaka 75 ambaye alichukua nafasi ya pili alipata 29%. Wawili hawa , kila mmoa ana imani mwamba atashinda uchaguzi huo.

George Weah, mtoto wa kijijini, aliyeibuka na kuwa mchezaji wa soka wa kimataifa katika miaka ya 1990 ana matumani makubwa ya kushinda uchaguzi. Mshambuliaji huyo wa PSG na AC Milan ni mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kushindia Golden mwaka 1995.

Hii ni mara ya tatu George Weah kuwania kinyang'anyiro hiki cha urais. Wafuasi wake wanasema kuwa kama alishindwa mwaka wa 2005 na 2011, ni kwa sababu ya wizi wa kura. Miaka mitatu iliyopita alichaguliwa Seneta wa Monrovia. Kwa 78% ya kura, alimdharau mpinzani wake, Robert Sirleaf, mtoto wa Rais Ellen Johnson Sirleaf, rais anayemaliza muda wake nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.