Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-UCHUMI

Rais mpya wa Zimbabwe kuunda serikali mpya

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajia kuunda serikali mpya anayoitaka na kuna taarifa kuwa tayari amevunja baraza la mawaziri lilokua likihudumu katika utawala wa mtangulizi wake Robert Gabriel Mugabe.

Emmerson Mnangagwa wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa, tarehe 24 Novemba 2017 katika uwanja wa mpira wa Harare.
Emmerson Mnangagwa wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa, tarehe 24 Novemba 2017 katika uwanja wa mpira wa Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mnangagwa ambaye aliapishwa siku ya Ijumaa Novemba 24, aliwahutubia wananchi wake, huku akiwataka kudumisha demokrasia.

Bw Mnangagwa alichukua hatamu ya uongozi wa Zimbabwe siku chache baada ya mtangulizi wake Robert Gabriel Mugabe kuachia ngazi kwa shinikizo la jeshi na chama chake kufuatia malumbano ndani ya chama chake kuhusu nani atakaemrithi.

Bw Mugabe alimfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa kwa kile mkewe Grace Mugabe alichokitaja kuwa alikua na njama za kutaka kumpindua mumewe katika uongozi wa nchi, madai ambayo Bw Mnangagwa alifutilia mbali na kusema ni uongo mtupu.

Haijafahamika iwapo baadhi ya mawaziri waliohudumu katiika serikali iliyotangulia watateuliwa katika serikali mpya. Lakini kinachofahamika tu ni kwamba aliekua waziri wa fedha katika serikali iliyotangulia na mshirika wa karibu wa Bw Mugabe anaendelea kushikilia kwa madai ya ubadhirifu wa mali ya umma na makosa mengine.

Robert Mugabe ambaye alijiuzulu kwenye uongozi wa nchi ya Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 93 atakua akilipwa mshahara wa dola 150,000 kila mwezi huku mkewe Grace Mugabe akilipwa nusu ya hizo, yaani dola 75,000. Mugabe vile vile amekubaliwa kupewa kiinua mgongo cha milioni 10,000,000, kwa mujibu wa gazeti la Guardian.

Robert Mugabena mkewe Grace katika sherehe ya kuadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake, Masvingo, kusini mwa Zimbabwe, tarehe 27 Februari 2016.
Robert Mugabena mkewe Grace katika sherehe ya kuadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake, Masvingo, kusini mwa Zimbabwe, tarehe 27 Februari 2016. REUTERS/Philimon Bulawayo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.