Pata taarifa kuu
MAREKANI-CLINTON-URUSI-SIASA

Hillary Clinton alaumu FBI na wadukuzi wa Urusi

Mgombea urais aliyeshindwa nchini Marekani na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, amewanyooshea kidole cha lawama wadukuzi wa Urusi na mkurugenzi wa Ujasusi nchini Marekani ambao walisababishwa anashindwa katika uchaguzi mkuu uliopita, nchini Marekani.

Hillary Clinton akiwalaumu wadukuzi wa Urusi na mkurugenzi wa Ujasusi nchini Marekani, James Comey waliosababishwa anashindwa katika uchaguzi wa urais.
Hillary Clinton akiwalaumu wadukuzi wa Urusi na mkurugenzi wa Ujasusi nchini Marekani, James Comey waliosababishwa anashindwa katika uchaguzi wa urais. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Bi Clinton alisema kwamba alikuwa amefanya kampeni nzuri na akapoteza kutokana na maswala yaliofanyika katika kipindi cha siku kumi za mwisho.

Hata hivyo amebaini kwamba amerudia katika ukumbi wa siasa na atahakikisha kuwa hatua yake hiyo inalenga kuweka upinzani mkali dhidi ya rais Trump ili kukosoa mambo mengi ambayo yanalenga kuididimiza Marekani katika sekta mbalimbali.

Itafahamika kwamba katika kampeni za uchaguzi wa urais, Donald trump alimkosoa kwa sera zake za kigeni na kutumia barua pepe za binafsi.

Bi Clinton ameelezea Bunge la Seneti mjini New York kwamba angeshinda kura hiyo iwapo uchaguzi huo ungefanyika tarehe 20 mwezi Oktoba kabla ya kuchapishwa kwa barua ya mkurugenzi wa FBI James Comey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.