Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-SIASA

Emmanuel Macron: FN ni chama kinachopambana dhidi ya Ufaransa

Mgombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron alimshambulia kwa maneno makali mpinzani wake Marine Le Pen alipokua akihutubia wafuasi wake 10,000 waliokusanyika katika eneo la La Villette, mjini Paris, siku ya Jumatatu Mei 1.

Emmanuel Macron alikishambulia chama cha National Front wakati wa mkutano wake wa kampeni katika eneo la La Villette, kaskazini mwa Paris, Mei 1, 2017.
Emmanuel Macron alikishambulia chama cha National Front wakati wa mkutano wake wa kampeni katika eneo la La Villette, kaskazini mwa Paris, Mei 1, 2017. RFI/Pierre René Worms
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa zimesalia siku sita kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais, mgombea wa En Marche! alitoa wito wa kuwa na "moyo wa kupambana" dhidi ya mrengo wa kulia, na kukishtumu chama cha National Front (FN)kuwa "chama kisichopenda Ufaransa".

Wagombea hawa wameendelea kurushiana vijembe ikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika Mei 7.

Wiki moja kabla ya duru ya pili ya Uchaguzi, Emmanuel Macron ameamua kutoka kwenye ukimya akionya dhidi ya cham cha FN, ambapo alikielezea kama chama kisio kisiopenda Ufaransa, "chama cha mawakala maafa," "chama cha kupambana Ufaransa. " Chama ambacho kimegubikwa na "kuwagawanya wananchi" na "kukuza chuki". Bw Macron alikwenda hadi kumtaja Bi Le Pen kama tu mwenye majivuno asiyependa wengine.

Emmanuel Macron, licha ya kushambuliwa na Le Pen Jumatatu katika mkutano wake wa kampeni katika mji wa Villepinte, amesema Marine Le Pen na chama chake cha FN wana lengo la kuitumbukiza Ufaransa katika hali ya machafuko.

Katika mkutano huo walikuepo, François Bayrou, Jean-Yves Le Drian na Ségolène Royal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.