Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA

Evan Mawarire kugombea uchaguzi Zimbabwe

Mchungaji wa Zimbabwe ambaye amekuwa akiongoza vuguvugu na maandamano ya kuipinga serikali ya rais Robert Mugabe, amesema kuwa huenda akagombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Mawarire licha ya kuachiwa kwa dhamana, anakabiliwa na mashataka ya kutatiza shughuli za Serikali na kuchochea wananchi kufanya vurugu.
Mawarire licha ya kuachiwa kwa dhamana, anakabiliwa na mashataka ya kutatiza shughuli za Serikali na kuchochea wananchi kufanya vurugu. MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mchungaji Evan Mawarire alitishwa hadharani na rais Mugabe punde tu baada ya kuanzisha vuguvugu la “This Flag” kupitia kwenye mtandao, vuguvugu ambalo lilisababisha maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Rais Mugabe ametangaza kuwa atawania tena urais kwenye uchaguzi mkuu jao na tayari chama chake cha ZANU-PF kimeshamuidhinisha kama mgombea wake.

Mawarire ambaye hivi sasa yuko nje kwa dhamana, anakabiliwa na mashitaka ya kutatiza shughuli za serikali na kuchochea wananchi kufanya vurugu.

Hata hivyo hajatangaza rasmi msimamo wake, ingawa amesema ikiwa muda utaruhusu kwa yeyekugombea urais ama akaombwa na wananchi wa Zimbabwe, basi atafikiria maombi hayo na huenda akaamua kusimama kama mgombea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.