Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Kesi ya uchaguzi wa Gambia kuskilizwa mwezi Mei

Mahakama ya juu nchini Gambia imetangaza kwamba inaahirisha kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya kura ya mwezi uliopita hadi mwezi Mei, kwa mujibu wa jaji mkuu wa Emmanuel Fagbenle.

Rais anayemaliza muda wake nchini Gambia Yahya Jammeh aendelea kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Gambia.
Rais anayemaliza muda wake nchini Gambia Yahya Jammeh aendelea kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Gambia. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files
Matangazo ya kibiashara

Wasuluhishi wa mzozo wa kisiasa nchini Gambia kutoka muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS walikutana mwanzoni mwa wiki hii mjini Abuja nchini Nigeria, kujadili hatima ya rais Yahya Jammeh ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika Uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita dhidi ya mpinzani wake Adama Barrow.

Bado haijulikani kitakachotokea baada ya muhula wa bwana Jammeh kukamilika tarehe 18 mwezi Januari.

Wakati huo huo aliyekuwa Waziri wa Habari nchini Gambia, aliyejiuzulu na kukimbilia nchini Senegal Sheriff Bojang, ametangaza kumuunga mkono Adama Barrow aliyetangazwa mshindi halali wa Uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita.
Waziri huyo wa zamani amesema amefikia uamuzi huo baada ya kusutwa na nafasi yake kutokana na kauli ya Jammeh kusema kuwa hataachia madaraka.

Aidha, amesema kuwa haamini kuwa Mahakama ya Juu itatoa uamuzi sahihi baada ya Jammeh, kuwasilisha kesi ya kutaka Uchaguzi huo kufutwa kwa madai kuwa uligubikwa na wizi wa kura.

Marais watatu wa nchi za Afrika Mashariki wanatarajiwa kuzuru Gambia Jumatano hii Januari 11, kuendeleza shinikizo za kumtaka Jammeh kuondoka madarakani kabla ya tarehe 19, siku ambayo muda wake wa kukaa madarakani utafika mwisho.

Umoja wa Mataifa, Mataifa ya Magharibi na Umoja wa Afrika, umemtaka Jammeh ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 22 kuheshimu haki za raia wa Gambia na kukubali kuondoka madarakani.

Wasuluhishi wa mzozo wa kisiasa nchini Gambia kutoka muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS walikutana mwanzoni mwa wiki hii mjini Abuja nchini Nigeria, kujadili hatima ya rais Yahya Jammeh ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika Uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita dhidi ya mpinzani wake Adama Barrow.

Mwenyekiti wa ECOWAS Ellen Johnson Sirleaf ambaye pia ni rais wa Liberia, mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa jijini Accra nchini Ghana, alisema muungano huo unafuatilia kwa karibu kinachofanyika nchini Gambia, na muungano huo utahakikisha kuwa uamuzi wa raia wa Gambia unaheshimiwa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambaye anaongoza ujumbe wa wasuluhishi hao, anatarajiwa kutoa mwelekeo wa namna mazungumzo yatakavyokuwa yamefikia baadaye siku ya Jumatatu.

Uamuzi kuhusu mgogoro huu wa Gambia, unastahili kufanyika kufikia tarehe 19 mwezi huu siku ya mwisho ya utawala wa rais Jammeh ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 22.

Ripoti zinasema kuwa, huenda jeshi la Senegal likaingilia kati na kumwondoa kwa nguvu rais Jammeh ikiwa atakataa kabisa kuondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.