Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Wanasiasa wa DRC watofautiana kuhusu uteuzi wa Samy Badibanga

Wanasiasa wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watofautiana kuhusu uteuzi wa Samy Badibanga kuiongoza serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambae anadaiwa kuwa mbuge wa upinzani kutoka chama cha UDPS katika kutekeleza makauliano yaliofikiwa kwenye mazungumzo ya wanasiasa wa nchi hiyo.

Samy Badibanga Septemba 1, 2016
Samy Badibanga Septemba 1, 2016 JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe ambae alikuwa amepewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo amesema wamepokea utauzi huo, kinachobaki ni kuendelea kufuatilia utekelezwaji wa yale yote yaliofikiwa kwenye mazungumzo hayo.

Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Septemba 1, 2016.
Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Septemba 1, 2016. JUNIOR D.KANNAH / AFP

Upande wake katibu mkuu wa chama cha UDPS Kabunda Kabunda amekanusha taarifa kwamba uteuzi wa kiongozi huyo utaathiri shughuli za chama cha Etienne Tchseketi badala yake amesema waziri mkuu huyo mpya sio mwanachama wa chama hicho kwa muda mrefu.

Naye Eve Bazaiba katibu mkuu wa chama cha MLC cha Jean Pierre Bemba Gombo amesema haifai kupotosha maswala yaliopo, na kwamba uteuzi wa serikali au waziri mkuu sio tatizo lililopo kwa sasa bali tatizo ni uheshimishwaji wa katiba.

Wakati huo huo Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRCongo litaendelea na mchakato wa kutafuta muafaka wa kisiasa kwa kukutana pande mbalimbali husika na mzozo huo.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewapongeza maaskofu walioanzisha mchakato huo wa kuunganisha pande zote na ambapo Ujumbe wake unatarajiwa kusomwa katika ibada ya misa ya makabisa ya kanisa hilo katoliki Jumapili hii.

Askofu Marcel Utambi Tapa mwenyekiti wa baraza hilo amesema uteuzi wa waziri mkuu na rais Joseph Kabila haumaanishi mwisho wa kuendelea na mchakato wa kutafuta maridhiano ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.