Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Kampeni za wagombea urais zaendelea Marekani

Zikiwa zimesalia siku zisizozidi kumi kabla ya uchaguzi, wagombea katika uchaguzo huo wanaendelea na kampeni zao katika majimbo mbalimbali, kila mmoja akitoa sera zake kwa kutafuta idadi kubwa ya sauti kabla ya uchaguzi huo kuanza mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Donald Trump na Hillary Clinton wakati wa mdahalo wao wa kwanza, Sempemba 26, 2016.
Donald Trump na Hillary Clinton wakati wa mdahalo wao wa kwanza, Sempemba 26, 2016. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump, anaendelea kuwa nyuma ya Bi Clinton kwenye kura za maoni katika majimbo mengine muhimu yanayoshindaniwa.

Wkati huo huo mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ataachana na kampeni kwa muda na kufungua jumba lake la hoteli ya Trump International lililo hatua chache kutoka ikulu ya White House.

Naye Hillary Clinton atatumia siku yake hii, ya kuadhimisha miaka 69 tangu kuzaliwa kwake, akifanya kampeni jimbo muhimu la Florida. Bi Clinton atakuwa na mikutano miwili katika jimbo la Florida.

Bw Trump atakata utepe katika hafla ya kuzindua jumba hilo Washington DC kisha arejelee kampeni katika jimbo la Carolina Kaskazini.

Hii ni hafla ya pili ya mauzo na utangazaji kwa mgombea huyo wiki hii.

Hoteli hiyo ya Bw Trump imegharimu Dola milioni 212 (sawa na Euro milioni 173) nai mejengwa eneo lililokuwa la posta ya zamani mjini Washington.

Mgombea mwenza wa Donald Trump, Mike Pence, atakuwa akiendesha kampeni yake katika jimbo la Utah. Jimbo hili halijaunga mkono mgombea urais wa chama cha Democratic katika kipindi cha miaka zaidi ya 50.

Mike Pence pia atasimama katika majimbo ya Nevada na Colorado kabla ya kuelekea katika jimbo lenye wafuasi wengi wa chama cha Republican la Nebraska Alhamisi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.