Pata taarifa kuu
IRAN-UCHAGUZI

Ahmadinejad ajiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania urais

Rais wa zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amechukua uamuzi Jumanne hii wa kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika 2017, kufuatia ushauri wa Kiongozi Mkuu Ali Khamenei.

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad mjini New York Septemba 26, 2012.
Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad mjini New York Septemba 26, 2012. REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Akitangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania urais, Mahmoud Ahmadinejad amekubali kutii amri ya Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei.

Kiongozi huyo Mkuu wa Iran alisema kuwa kugombea kwa Mahmoud Ahmadinejad katika uchaguzi wa urais wa Mei 2017 ni kinyume na maslahi ya taifa, kwa sababu angelisababisha madhara ya ubaguzi wa kisiasa.

Rais wa sasa mwenye msimamo wa wastani Hassan Rouhani anatarajiwa kugombea kwa muhula wa pili mwaka 2017.

Pamoja na kujiondoa kwa Mahmoud Ahmadinejad, chama cha Conservative kitajaribu kuunganisha safu yake kwa kuwasilisha mgombea mmoja dhidi ya Hassan Rohani, ambaye anaungwa mkono wafuasi wa vyama vinavyotaka mabadiliko, ambao ni wenye msimamo wa wastani.

Mgombea wa urais wa zamani Ahmadinejad hangelisababisha tu ubaguzi wa kisiasa nchini, lakini pia angelisababishwa mgawanyiko miongoni mwa wafuasi wa chama cha Conservative.

Wakati wa mihula yake miwli ya uongozi kati ya mwaka 2005 na 2013, rais wa zamani wa Iran Ahmadinejad alikuwa maarufu kwa sera zake dhidi ya mataifa ya magharibi na dhidi ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.