Pata taarifa kuu
BRAZIL-LULA

Lula atuhumiwa kuwa "kiongozi mkuu" wa mtandao wa rushwa

Nchini Brazil, mwendesha mashitaka anayehusika na uchunguzi wa kashfa ya rushwa katika kampuni ya umma ya mafuta ya Petrobras, aliomba Jumatano, Septemba 14 kushtakiwa kwa rais wa zamani Lula kwa rushwa na kujitajirisha kinyume cha cheria.

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Marisa Leticia Agosti 15, 2016 katika mji wa Sao Paulo.
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Marisa Leticia Agosti 15, 2016 katika mji wa Sao Paulo. REUTERS/Paulo Whitaker
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mashambulizi ya moja kwa moja na mabaya zaidi kuelekezwa dhidi ya Lula. "Leo hii, Mwendesha mashitaka mkuu anamtuhumu Bw Luiz Inacio Lula da Silva kuwa kiongozi mkuu wa rushwa kuhusiana na uchunguzi uliyopewa jina la Lava Jato [uoshaji wa haraka], " amesema mwendesha mashitaka, Deltan Dallagnol.

Anamshutumu rais wa zamani wa mrengo wa kushoto kuwa ni "kiongozi mkuu wa uhalifu wa rushwa" unaohusiana na kampuni kubwa ya umma ya mafuta Petrobras, jina lililopewa kashfa hiyo ya rushwa iliyoibuka katika miaka mitatu iliyopita, lakini ingekuwa imeanza chini ya utawala wa Lula, wakati mwenyewe aliteua wakurugenzi wa kampuni ya Petrobras wanaohusika na kuhudumia mtandao mkubwa wa rushwa.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka, ambaye amewakilisha faili hiyo katika mahakama kwa minajili ya kufunguliwa mashtaka yeye na mkewe Marisa Leticia, wawili hao wanahusika moja kwa moja na kashfa hii.

Lula anatambulika kama mkuu katika uongozi wa uhalifu, na ambaye alikua akiratibu utekelezaji wake. " Euro milioni moja ilitolewa katika neema yake, " kwa mujibu wa mwendesha mashitaka.

Kwa upande wa wafuasi wa rais wa zamani, shutuma hizi ni mbinu za kumkamata Lula, wiki mbili baada ya kuondolewa mamlakani Dilma Rousseff, ambalye alimrithi Lula katika uongozi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.