Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI

Mkutano wa kwanza wa Tshisekedi tangu mwaka 2011

Mamia kwa maelfu ya wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyoungana na chama cha UDPS wamekusanyika Jumapili hii katika uwanja wa mpira wa Stade de Martyr mjini Kinshasa. Mkutano huu wa upinzani ni wa kwanza kufanyika tangu mwanzoni mwa mwaka huu, pia ni wa kwanza kwa Etienne Tshisekedi.

Etienne Tshisekedi akiwa jukwani akiwahotubia wafiasi wake tangu mwaka 2011.
Etienne Tshisekedi akiwa jukwani akiwahotubia wafiasi wake tangu mwaka 2011. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha UDPS amewahutubia wafuasi wake na wale kutoka vyama vingine vya upinzani, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011.

Vyama vyote vinavyoungana na chama cha UDPS vilikuepo, ikiwa ni pamoja na UDPS bila shaka, muungano wa G7, G14 pamoja na wajumbe wa shirika la kiraia la LUCHA, ambao walikua na bango lililoandikwa "tunaomba kuachiliwa huru kwa wanaharakati wetu pamoja na wafungwa wa kisiasa."

Mkutano huo ulianza saa 3 asubuhi hadi saa tisa alaasiri. Bw Tshisekedi, ambaye ni mpinzani wa kihistoria aliondoka nyumbani kwake akishindikizwa na maelfu ya wafuasi wake ambao walijiunga na wengine waliokua wakimsubiri katika uwanja wa mpira wa Stade de Martyr.

Kabla ya hotuba yake, Etienne Tshisekedi amewataka raia kusalia kimya kwa muda wa dakika moja ili kuwakumbuka wale walio katika matatizo, hasa katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Etienne Tshisekedi alitoa ujumbe kwa Rais Joseph Kabila akimtaka kuondoka mamlakani Desemba 20, atakapokua amemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho. Pia ameomba wajumbe wa Tume ya Uchaguzi (CENI) kujiuzulu haraka iwezekanavyo ifikapo mwezi Septemba.

Wakati huo huo Moise Katumbi Chapwe, mkuu wa zamanai wa mkoa wa zamani wa Katanga, pia aliye kuwa mshirika wa karibu wa Rais Joseph Kabila Kabange, katika tangazo alilolitoa Jumapili usiku, amesema anakaribisha hotuba ya Etienne Tshisekedi.

Nilitaka kurejea katika nchi yangu na kushiriki katika mkutano huo, licha ya vitisho vya kukamatwa viliyotolewa dhidi yangu na Waziri wa Sheria. Kwa bahati mbaya, serikali imenikatalia kurudi nchini baada ya ndege yangu kunyimwa ruhusa ya kutua katika uwanj wa mjini Kinshasa. Nalaani kwa mara nyingine tena uamuzi huu usiofuata sheria, ambao unaonyesha jinsi gani uhuru wa raia unadidimizwa katika nchi yetu.

Utawala unanitishi kunikamata kwa uhalifu ambao sikuweza kufanya na ambapo nilihukumiwa na mahakama inayotumiwa na utawala huo. Mbali na kunidhoofisha, mbinu hizi zinaniimarisha katika mapambano yangu ya amani ili kuweka utawala wa sheria. Utawala wa kiimla na uzembe hauna nafasi katika nchi yetu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.