G7-UINGEREZA-UCHUMI
G7 yaisihi Uingereza kutojoundoa katika EU
Viongozi wa mataifa yaliyoendelea kiwanda duniania ya G7 wameafikiana kwa pamoja kuunga mkono Uingereza kutojiondoa katika Umoja wa Ulaya EU.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Viongozi hao wanaokutana nchini Japan wamesema kuondoka kwa Uingereza katika umoja huo kutayumbisha uchumi wa dunia.
Wananchi wa Uingereza tarehe 23 mwezi ujao watapiga kura, kuamua ikiwa wanataka kuendelea kuwa katika Umoja huo au kuondoka.
Waziri Mkuu David Cameron amekuwa akifanya kampeni kuwahimiza Waingereza kupiga kura ya kusalia katika umoja huo.
Mbali na suala la Uingereza, viongozi hao wamezungunzia maswala mengine kama ugaidi, uchumi na suala la wakimbizi.