Pata taarifa kuu
GAMBIA-SENEGAL-MGOGORO

Gambia na Senegal zashindwa kutatua mgogoro wa mpaka wao

Gambia na Senegal wameshindwa, wakati wa duru ya kwanza ya mfululizo wa mazungumzo ya Jumapili mjini Dakar, kutatua mgogoro wa mpaka unaodhoofisha nchi hizi mbili kwa miezi mitatu, Mshauri kwenye wizara ya mambo ya Nje ya Senegal amebaini.

Des voyageurs passent la frontière entre la Gambie et le Sénégal à Keur Ayip, le 9 mai 2016.
Des voyageurs passent la frontière entre la Gambie et le Sénégal à Keur Ayip, le 9 mai 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo serikalini amehakikisha kwamba mazungumzo yatendelea tena ndani ya kipindi cha miezi miwili. "Mkutano ujao utafanyika mwezi Julai," afisa hyo asema, wakati ambapo nchi hizi mbili tayari zimeanza kukabiliwa na uhaba wa baadhi ya bidhaa mahijio.

Jumapili mjini Dakar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Neneh McDouall-Geye alikutana kwa saa kadhaa na mwenzake wa Senegal, Mankeur Ndiaye, ili kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro huu uliyoanzisha na wamiliki wa magari ya uchukuzi kutoka Senegal tangu katikati ya mwezi Februari.

Watu hawa wameendelea kuzuia mpaka na Gambia, nchi ndogo inayozungukwa na Senegal, ili kupata mazingira mazuri kwa kuweza kuingia katika nchi hiyo.

Mgogoro uliibuka mapema mwezi Februari kutokana na kuzidisha mara mia moja ada ya kiingilio kilichowekwa na Gambia kwa malori yanapita nchini humo.

Vyama vya wachukuzi kutoka Senegal, hivi karibuni, vililiambia shirika la habari la AFP kwamba wasingeweza kuondoa vikwazo hivyo iwapo watakua bado hawajapata ufunguzi wa kudumu wa mpaka, unaofungwa kila siku saa 1:00 usiku hadi saa 1:00, asubuhi, na mafanikio makubwa katika mradi wa ujenzi wa daraja kwenye Mto Gambia. Daraja Hili litaepusha magari ya uchukuzi kutoka Senegal kufanya mwendo mrefu wa mamia ya kilomita kwa kusafiri kati ya kusini na kaskazini mwa nchi hiyo.

"Tutashauriana na wataalam wetu juu ya suala la daraja," Mshauri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Senegal ameliambia shirika la habari la AFP, na kuhakikisha kwamba Dakar itashirikiana na "wamiliki wa magari ya uchukuzi" kwa kufungua upya mpaka huo kwa wafanyabiashara".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.