Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-UCHUMI

Dilma Rousseff kuwekwa kando ya mamlaka

Dilma Rousseff anasalia labda na masaa yake ya mwisho katika uongozi wa nchi ya Brazil. Maseneta wanajiandaa Jumatano hii kumng'atua mamlakani kwa muda, na kumuweka katika kesi ya kumtaka ajiuzulu kutokana na kutumia kinyume cha sheria akaunti za umma.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Mei 6, 2016, katika Ikulu ya Planalto, Brasilia.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Mei 6, 2016, katika Ikulu ya Planalto, Brasilia. AFP
Matangazo ya kibiashara

Muhula wa pili wa rais mwenye umri wa miaka 68, kutoka chama cha mrengo wa kushoto, ambaye amepoteza imani kwa wananchi wake unaonekana kukabiliwa na hali ngumu, baada ya serikali kuwasilisha rufaa kwa Mahakama Kuu ya nchi hiyo (STF), ikiomba kufuta utaratibu wa kujiuzulu kwa Rais Dilma Rousseff.

Rais wa Brazil na serikali yake wamewasilisha rufaa hiyo Jumanne kwa mahakama ya juu, wakiomba kufuta kile walichokitaja kama "mapinduzi" ya kitaasisi "bila kutumia silaha wala kifaa chochote cha jeshi."

Maseneta wameitishwa kuanzia saa 3:00 asubuhi (sawa na saa 6:00 mchana saa za kimataifa) katika kikao cha pamoja kuamua juu ya ufunguzi rasmi wa mashtaka ya kesi ya kung'atuliwa kwa Bi Rousseff, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa nchi kubwa katika Amerika ya Kusini mwaka 2010.

Matokeo ya kura, yanatarajiwa, bila shaka, kutangazwa Jumatano hii jioni au usiku.

Maseneta hamsini kwa jumla ya 81 walitoa msimamo wao katika neema ya ufunguzi wa kesi ya Dilma Rousseff, mpiganaji wa zamani wa vita vya maguguni aliyeteswa na kufungwa chini ya utawala wa udikteta wa kijeshi. Kura 41 ndizo zinahitajika ili utaratibu ho wa kumuweka Bi Rousseff kando ya wadhifa wake utekelezwe.

- 'Uhalifu wa kimajukumu' -

Isipokuwa kwa mshangao mkubwa, Rousseff anatazamiwa moja kwa moja kutengwa katika uatawala kwa kipindi kisichozidi siku 180, kwa kusubiri uamuzi wa mwisho wa Maseneta, ambao unaweza kutolewa mwezi Septemba.

Iwapo jambo hilo llikifaulu, nafasi ya B Rousseff itachukuliwa Ijumaa wiki hii na mshirika wake wa zamani aliyegeuka mpinzani, Makamu wa Rais Michel Temer, 75, kiongozi wa chama kikubwa cha mrengo wa kati cha PMDB, ambapo chama hicho kilijiondoa katika muungano wake mwishoni mwa mwezi Machi.

Iwapo Bi Rousseff ataondolewa mamlakani moja kwa moja, nafasi hiyo itachukuliwa na Michel Temer hadi uchaguzi mkuu ujao (urais na wabunge), uliopangwa kufanyika mwaka 2018.

Upinzani anamtuhumu rais kuwa alitenda "uhalifu wa kimajukumu" ambao unamsababishia kuondolewa mamlakani kwa mujibu wa katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.