Pata taarifa kuu
DJIBOUTI-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais wafanyika Djibouti

Raia wa Djibouti wanapiga kura leo Ijumaa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais. Rais Ismail Omar Guelle, madarakani kwa miaka 17 sasa, ni mgombea katika uchaguzi huo, pamoja na ahadi alizozitoa lakini hajazitekeleza.

Rais wa Djibouti, Ismaïl Omar Guelleh, apewa na fasi ya kushinda uchaguzi wa urais wa Ijumaa Aprili 8.
Rais wa Djibouti, Ismaïl Omar Guelleh, apewa na fasi ya kushinda uchaguzi wa urais wa Ijumaa Aprili 8. AFP/Jim Watson
Matangazo ya kibiashara

Katiba inamruhusu kugombea tangu kufanyika marekebisho ya 2010, ambayo yaliondoa kikomo kwa idadi ya mihula. Uchaguzi usio kuwa na mashaka kwani anapewa nafasi kubwa ya kushinda hasa kwa sababu ya mgawanyiko ndani ya upinzani.

Miongoni mwa wagombea, wengi ni wale ambao wanashtumu "kuingiliwa" katika kampeni zao. Wengine wana hofu kulifanyika makosa katika maandalizi ya uchaguzi, ambao unampa na fasi ya kushinda Ismail Omar Guelleh.

Wagombea vigogo wa upinzani ni Omar Elmi Kaireh na Mohamed Daoud Chehem, lakini kwa sababu ya kutokuwa na umoja miongoni mwao, watakuwa na kibarua kigumu kuung'oa utawala wa rais Ismael Omar Guelleh ambaye yupo madarakanitangu 1999.

Rais Guelleh ni rais wa pili tu tangu nchi hiyo ijikomboe kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa mwaka wa 1977.

Chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa kimesema kutiwa wasiwasi na jinsi uchaguzi ulivyoandaliwa. Chama cha Rais Hollande kimeonyesha wake kuhusu uchaguzi huo. Chama cha PS kinatolea wito "mashirika ya kimataifa (...) kuchukua msimamo ulio imara (...) na kutoa kauli moja kwa kuandaa uchaguzi wa kweli."

Tangazo hilo linauomba Umoja wa Afrika, uliopeleka timu ya waangalizi nchini humo, wawakilishi wa Umoja wa Kiarabu, IGAD (Mamlaka baina ya serikali kuhusu Maendeleo) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kufanya kuchukua msimamo thibiti.

Wiki hii, timu ya wanahabari wa BBC walikamatwa na kufukuzwa bila hata hivyo serikali kutoa maelezo. Djibouti imewekwa na Shirika la Wanahabari wasio na mipaka (RSF) kwenye nafasi ya 170 kwa nchi 180 katika suala la uhuru wa habari. Kama mamlaka inasema kuwa na imani na imeridhika na maandalizi ya uchaguzi, wengi wana hofu ya kukiukwa kwa utaratibu wa uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.