Pata taarifa kuu
ASTRALIA

Waziri Mkuu wa Australia aokolewa na Vikosi vya Usalama kutoka kwa Waandamanaji wenye hasira

Kikosi cha Usalama nchini Australia kilijikuta kinapata kazi ya ziada ya kuweza kumuokoa Waziri Mkuu Julia Gillard na Kiongozi wa Upinzani Tonny Abbott waliokuwa kwenye Mgahawa wa Canberra baada ya kuzungukwa na waandamanaji wenye hasira.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao wenye ghadhabu walikuwa kwenye maandamano ya kukumbuka kuondoka kwa Wakulima Wakubwa wa Kiingereza ambao walikuwa wanamiliki mashamba mnamo mwaka 1788.

Gillard na Abbott walilazimika kuondolewa wakiwa chini ya ulinzi mkali uliokuwa unaongozwa na kikosi maalum cha kuzuia ghasia ili kuwaepusha na hasira za waandamanaji hao.

Kwenye harakati hizo la kujiepusha wa waandamanaji hao Waziri Mkuu Gillard alishuhudiwa akianguka chini wakati akiendelea na juhudi zake za kujiepusha na watu hao wasimdhuru kabla ya kupatiwa msaada wa Kikosi cha Usalama.

Waziri Mkuu Gillard amekiri kuchangazwa ni tukio hilo lililotekelezwa na waandamanaji nchini Australia na kusema hajui sababu za watu hao kudiriki kumshambulia yeye na Kiongozi wa Upinzani Abbott.

Kiongozi huyo amewapongeza Wanausalama baada ya kufanikisha kumuokoa kutoka kwenye mikono ya waandamanaji wenye hasira ambao wamechukizwa na kauli ya Abbott ambaye amesema siku hiyo haina maana tena kwatika miaka hii.

Waandamanaji hao wakichagiwa na nyimbo ambazo walikuwa wanaimba wakisema “aibu” na “ubaguzi” wanatajwa kufanya fujo ambazo zimechangia kuharibu jengo la Mgahawa wa Canberra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.