Pata taarifa kuu
Japan

Waziri Mkuu wa Japan apigiwa kura ya kuwa na imani nae

Jaribio la kutaka kumuangusha Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan, kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae limegonga mwamba, baada ya kiongozi huyo wa serikali kushinda kwa kishindo, na kuwaacha midomo wazi mahasimu wake wa kisiasa. 

Waziri mkuu wa Japan Naoto Kan, baada ya kupigiwa kura ya kuwa na imani nae, bungeni.
Waziri mkuu wa Japan Naoto Kan, baada ya kupigiwa kura ya kuwa na imani nae, bungeni. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu huyo, ameweza kuvuka kizuizi hicho ambacho kililenga kuipima serikali hiyo ambayo inakabiliwa na kibarua kigumu, cha kulijenga taifa hilo upya baada ya kukumbwa na tetemeko la chini ya bahari.

Muswada wa kupiga kura hiyo, ulipelekwa bungeni na Chama Kikuu cha Upinzani LDP, kikishirikiana na vyama vingine vya kisiasa.

Katika zoezi hilo, Waziri Mkuu Kan amefanikiwa kupata kura mia mbili tisini na tatu, dhidi ya mia moja hamsini na mbili, ambazo zilimpinga na hivyo kukipa dhamana chama hicho kuendelea kushika usukani.

Mapema kabla ya kupigiwa kura, Kan alisema hawezi kuondoka hadi ahakikishe, ameijenga Japan sawasawa, nchi ambayo imepatwa na janga la nyuklia mwzi Machi, na kusababisha uvujaji wa mionzi katika mtambo wa Fukushima Daichi.

Aidha, Mtu wa Watu, kama anavyojulikana zaidi, ameahidi kuwa serikali yake itakuwa mstari wa mbele kuwapatia makazi ya muda watu zaidi ya laki moja ambao wameathirika na madhara ya tsunami hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.