Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia 2022: Cameroon wailaza Brazil 1-0 lakini washindwa kufuzu

Vincent Aboubakar, nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Camzeroon, mfungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika, ambaye aliishangaza Brazil kwa bao la kichwa.

Raia wa Cameroon wakishangilia bao la dakika za lala salama la Vincent Aboubakar (n°10), mnamo Desemba 2, 2022 dhidi ya Brazil.
Raia wa Cameroon wakishangilia bao la dakika za lala salama la Vincent Aboubakar (n°10), mnamo Desemba 2, 2022 dhidi ya Brazil. REUTERS - DYLAN MARTINEZ
Matangazo ya kibiashara

Kupambana hadi mwisho, Vincent Aboubakar aliheshimu hadhi yake kama nahodha dhidi ya Brazil (1-0), akiipa Cameroon ushindi wa hali ya juu lakini usiotosha kujiunga katika mzinguko wa nane, siku ya Ijumaa katika michuano ya Kombe la Dunia-2022, kabla ya kuondolewa ncje ya uwanja kwa kuvua jezi yake baada ya kufunga bao lake.

Mchezaji wa akiba katika mechi mbili za kwanza, mshambuliaji wa Al-Nassr, Saudi Arabia, alijikakamua, akijua alipunguzwa kasi na goti dhaifu.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Porto, mfungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika nyumbani mwaka 2022 (mabao nane), kwa upande wake alikimbia kuelekea kwenye nguzo kwa kuvua jezi yake, akiwa amelewa kwa furaha.

Lakini wakati wake ulikuja nchini Qatar na bao lake, la kichwa litakumbukwa katika dakika 90 + 2, ambalo lilikatisha kasi ya Brazil, moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hii.

Mwamuzi alilazimika kumpa kadi ya njano ya pili, sawa na nyekundu, na Cameroon ikamaliza mchezo bila yeye.

Lakini hilo halikuwa jambo kuu. Ni wazi, ushindi huu haukubadilisha chochote, wala kwa Brazil, iliyofuzu katika mzunguko wa nane, wala kwa Cameroon, iliyoondolewa.

Simba wa Nyika walijivunia kuwa tayari waliifunga Brazil, kwenye michuano ya Michezo ya Olimpiki ya 2000 au michuano ya Kombe la shirikisho la mwaka 2003? Walifanya hivyo tena Ijumaa huko Qatar, kwa mtindo safi kabisa wa kile kocha wao Rigobert Song alichokiita baada ya mechi “roho ya Simba”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.