Pata taarifa kuu

Kombe la dunia 2022: Senegal yatinga katika mzunguko wa 8 kwa kuifunga Ecuador 2-1

Baada ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kuandikisha ushindi katika michuano ya Kombe la Dunia la 2022, mabingwa wa Afrika Senegal wamedhihirisha ubabe wao dhidi ya Ecuador Jumanne kwa ushindi wa 2-1 ambao uliifanya Simba ya Teranga kutinga katika mzunguko wa nane. Kwa pointi 7, Uholanzi wanaongoza Kundi A.

Kalidou Koulibaly ameifungia Senegal bao la pili.
Kalidou Koulibaly ameifungia Senegal bao la pili. REUTERS - DYLAN MARTINEZ
Matangazo ya kibiashara

Bao la kwanza lmefungwa na Ismaïla Sarr dakika ya 44 kwa penalti. Matokeo wakati wa mapumziko Senegal ilikuwa inaongoza kwa 1-0.

Wakiwa wamerudi kutoka chumba cha kubadilishia nguo, Ecuador walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 67, kwa bao lililopachikwa wavuni na Moisés Caicedo.

Mbali na kukata tamaa, Simba wa Teranga walirejea kwa nguvu na kuishia kupata bao la pili lililofungwa na Kalidou Koulibaly dakika ya 70.

Matokeo ya mwisho: 2-1.

Wakiwa na pointi 7, Uholanzi wanaongoza kundi A baada ya kuwalaza wenyeji Qatar mabao 2-0.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.