Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia: Senegal "mgongo ukutani" dhidi ya Qatar (Cissé)

Senegal, iliyochapwa 2-0 na Uholanzi katika mechi yake ya kwanza katika michunao ya Kombe la Dunia-2022, tayari imeanza "kujifikiria mengi tu" lakini inaweza kutegemea "uzoefu wake wa pamoja" kabla ya kukabiliana na Qatar siku ya Ijumaa, amesema kocha Alious Cisse Alhamisi.

Aliou Cissé, kocha wa Simba ya Teranga.
Aliou Cissé, kocha wa Simba ya Teranga. SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi mwenyeji, ambayo pia ilibwagizwa mabao 2-0 na Ecuador katika mechi ya ufunguzi, lazima sasa "ionyeshe kiwango chake cha kweli", aamebaini kocha wa Qatar Félix Sanchez.

Aliou Cissé (kocha wa Senegal): "Ni mechi muhimu sana kwa timu zote mbili. Katika mashindano ya kiwango hiki, kutoka wakati unapoteza mechi yako ya kwanza, huwa unafikiria kupoteza tena au kufanya vizuri mechi ya pili. Lakini (katika) uzoefu wetu wa pamoja, (kuna) mechi nyingine ambazo tulipaswa kucheza ambazo zilikuwa katika kiwango hiki cha nguvu, shinikizo, umuhimu na mahitaji. Ni kwetu sisi kupambana kwa minajili ya kufanya vizuri na kujikumbusha kila kitu tulichofanya siku za nyuma wakati tumekuwa katika hali kama hiii."

Félix Sanchez (kocha wa Qatar): "Kuingia kwetu kwenye mashindano hakukuwa vile tulivyotarajia. Mbali na matokeo, tungependa kuwa na ushindani zaidi. Pengine tulikuwa na woga kidogo na hiyo iliathiri utekelezaji na kufanya maamuzi. mechi ijayo, tutajaribu kuonyesha kiwango chetu cha kweli, ambacho wale waliotuona tunacheza wanakijua. Lakini pia kuna wajibu wa matokeo kwa timu nyingine."

Kalidou Koulibaly (beki na nahodha wa Senegal): "Tupo hatarini kupoteza mechi ijayo lakini hapo ndipo tutawaona simba wa kweli. Tunajua kwamba tuna uwezo wa kufanya vizuri katika mechi hizi mbili (dhidi ya Qatar kisha Ecuador. ) kucheza fainali mbili kujaribu kuchukua pointi sita, hata kama tunajua itakuwa vigumu. Tutatoa kilio chini ya uwezo wetu kesho (Ijumaa) ili kuweza kufanya vizuri na kuwafurahisha Wasenegal."

Ismaeel Mohammad (beki wa Qatar): "Hatua ya kwanza ni kuweka mambo kwa vitendo uwanjani. Ikiwa hatujafaulu (wakati wa mechi ya uzinduzi), tuna nafasi nyingine. Kupita kwenye awamu ya makundi inabaki kuwa lengo kuu kwetu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.