Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Wanachi wa Senegal kuipokea timu yao kwa vifijo na nderemo baada ya ushindi

Raia wa Senegal wameendelea kusherehekea usiku kucha kuamkia Jumatatu katika miji mbalimbali nchini Senegal kufuatia ushindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Idrissa Gana Guèye na mabingwa wapya wa Senegal wa Afrika.
Idrissa Gana Guèye na mabingwa wapya wa Senegal wa Afrika. © Pierre René-Worns
Matangazo ya kibiashara

Video zinaonesha mashabiki wa timu hiyo wakiwa wanapeperusha bendera ya taifa hilo wakiwa wanacheza densi pamoja na ujumbe kutoka kila pembe uliokuwa unamiminika kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza Jumatatu kuwa siku ya mapumziko kusherehekea ushindi wa timu ya taifa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Rais ambaye alikuwa nje ya nchi amefutilia mbali awamu ya mwisho ya safari yake ili kuwakaribisha nyota hao wa soka kurejea nchini siku ya Jumatatu.

Rais Sall ataitunuku timu hiyo Jumanne katika ikulu ya rais, televisheni ya RTS ilisema.

Senegal ilishinda Misri 4-2 kwa mikwaju ya penalti na kupata ushindi wao baada ya fainali kumalizika bila bao kufuatia muda wa nyongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.