Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

AFCON 2022: Senegal yatinga fainali baada ya kuiburuza Burkina Faso

Senegal imefuzu katika fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kuilaza Burkina Faso kwa mabao 3-1

Burkina Faso yaburuzwa kwa mabao 3-1 na Senegal katika nusu fainali ya michuano ya AFCON 2022.
Burkina Faso yaburuzwa kwa mabao 3-1 na Senegal katika nusu fainali ya michuano ya AFCON 2022. © FMM/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Bao la kwanza la Senegal lilipachikwa kimyani na Abdou Diallo katika kipndi cha pili cha mchezo.

Bao la pili lilipatikana dakika ya 76 kupitia mchezaji Idrissa Gueye baada ya kupewa pasi safi kutoka kwa Sadio Mane. Dakika chache baadae Mane alihitimisha ushindi wa Senegal kwa kupachika bao la tatu. Lilikuwa goli la 29 la Mane kwa taifa lake , na kumuweka sawa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Henry Camara.

Senegal  itakabiliana na Misri katika fainali au waandaji wa dimba hilo Cameroon katika fainali ya siku ya Jumapili.

Burkina Faso nayo itashiriki katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambayo yitachezwa siku moja kabla ya fainali hiyo.

Nani atakaye twaa kombe mwaka huu kati ya timu tatu zinazosalia

Misri na Cameroon ni nchi mbili zenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya AFCON, Misri ikiwa ni mabingwa mara saba na Cameroon wameshinda kombe mara tano. Timu ya Senegal ama ikijulikana zaidi kama Simba wa Teranga wanatafuta kushinda kombe hilo, miaka miwili baada ya kupoteza dhidi ya Algeria katika fainali ya mjini Cairo.

Shirikisho la soka afrika CAF, limesema mechi ya kuwania nafasi ya tatu ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachezwa Jumamosi hii, Februari 5. Awali mechi hiyo ilikuwa imepangwa kupigwa saa tatu kabla ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili, lakini sasa itachezwa Jumamosi saa nane mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.