Pata taarifa kuu

AFCON 2022: Motsepe ataka maelezo baada ya mkanyagano uliotokea katika uwanja wa Olembé

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amefanya mkutano wa kipekee na waandishi wa habari Jumanne Januari 25 katika uwanja wa Ahmado-Ahidjo, siku moja baada ya mkanyagano uliosababisha vifo vya takriban watu wanane kwenye uwanja wa Olembé kabla ya mechi ya AFCON kuanza. Kiongozi huyo ametangaza hatua kadhaa na kuomba ripoti ya haraka kuhusu hali ya mkasa huo.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), akionea katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne Januari 25 katika uwanja wa Ahmado-Ahidjo, siku moja baada ya mkanyagano uliosababisha vifo vya takriban watu wanane kwenye uwanja wa Olembé
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), akionea katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne Januari 25 katika uwanja wa Ahmado-Ahidjo, siku moja baada ya mkanyagano uliosababisha vifo vya takriban watu wanane kwenye uwanja wa Olembé AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Rais wa CAF anajikuta akikabiliana na mgogoro mkubwa. Watu wanane wamefariki dunia na hamsini kujeruhiwa, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya.

Baada ya kuwatembelea waathiriwa asubuhi, Patrice Motsepe amezungumza na waandishi wa habari mapema Jumanne mchana. Alianza kwa kukaa kimya kwa muda wa dakika moja kabla ya kutuma rambirambi zake kwa famia za waliojeruhiwa au waliofariki siku Jumatatu katika mkasa huo.

Hakutakuwa na mechi kwenye uwanja wa Olembe Januari 30

Kiongozi huyo wa CAF, kutoka Afrika Kusini ametangaza hatua ya kwanza muhimu: hakutakuwa na robo fainali katika uwanja wa Olembé siku ya Jumapili, Januari 30. Mechi hii, ambayo itakutanisha mshindi kati ya Côte d'Ivoire na Misri dhidi ya mshindi kati Morocco na Malawi, imehamishiwa kwenye uwanja wa Ahmadou-Ahidjo huko Yaoundé.

Mkutano na kamati ya maandalizi ya AFCON (COCAN) umepangwa kufanyika Jumatano tarehe 26 Januari. Katika hafla hii, Patrice Motsepe atatoa ombi lingine kuhusiana na mechi nzingine: robo fainali iliyopangwa kupigwa katika uwanja wa mjini Douala Januari 30 (mshindi kati ya Senegal na Cape Verde dhidi ya mshindi kati ya Mali na Equatorial Guinea) iweze kuhamishiwa Limbe.

Kwa upande wa usalama, rais wa CAF anatoa wito wa "hatua za haraka kuhakikisha hili halitokei tena". "Tunapaswa kuamua majukumu", anasema, lakini anaongeza kuwa "huu sio wakati wa kunyoosheana kidole", wala kila mmoja kukimbia "majukumu" yake: "Kisheria, serikali ya Cameroon inawajibika kwa usalama. Lakini sisi ni washirika wake. (…) CAF ni mshirika na tunawajibika kama mamlaka ya Cameroon. »

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.