Pata taarifa kuu
SOKA-EURO 2020

Kufa kupona kwa timu za kundi F kwenye michuano ya EURO 2020

Ureno itaanza kampeni yake ya kutetea taji la Euro dhidi ya Hungary jijini Budapest. Mshamulizi Cristiano Ronaldo mwenye umri wa 36, na mlinzi Pepe mwenye umri wa 38, ni miongoni mwa wachezaji waliyoshinda taji hili mwaka 2016. Wakati huo huo Ufaransa anashuka dimbani kumenyana na Ujerumani katika kundi hilo linaloitwa na mashabiki kuwa kundi la kifo.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wakichanganyikana na mashabiki baada ya bao la pili la Antoine Griezmann dhidi ya Ujerumani Julay 7 2016
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wakichanganyikana na mashabiki baada ya bao la pili la Antoine Griezmann dhidi ya Ujerumani Julay 7 2016 © AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

 

Siku ya Jumapili maandalizi ya Ureno yalipata pigo baada ya mlinzi wa Manchester City Joao Cancelo kupatikana na virusi vya Covid-19 hali iliyomlazimu kuondoka kwenye kambi. Nafasi yake sasa imechukuliwa na mchezaji wa  Manchester United Diogo Dalot.

Kikosi cha Ureno kina wachezaji tisa wanaosakata kandanda katika ligi kuu ya Uingereza. Wao ni kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes, mshambulizi wa Liverpool Diogo Jota, Ruben Dias na Bernardo Silva wa Manchester City pamoja na wachezaji wanne wa Wolves; Rui Patricio, Nelson Semedo, Joao Moutinho na Ruben Neves.

Ureno  wanashiriki kwa mara ya nane katika mashindao haya na watarajibu kuwa timu ya pili kutetea ubingwa wao baada ya Uhispania (2008, 2012).

Hungary, iliyomaliza ya tatu katika mashindano haya 1964 watakuwa wakishiriki katika mchuano huu kwa mara ya nne. Mwaka 2016 waliondolewa katika hatua ya 16 bora; waliorodheshwa kwenye kundi moja na mechi kati yao iliishia sare ya 3-3.

Ujerumani Vs Ufaransa

Uwanjani Allianz Arena Ujerumani itaikaribisha Ufaransa katika mechi ya pili ya kundi F. Ufaransa ambao ni mabingwa wa kombe la dunia, wana matumanini katika mechi ya leo baada ya Karim Benzema na Antoine Griezmann kupona majeraha waliyoyapata katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bulgaria wiki iliyopita.

Kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka atakosa mechi ya leo kwani bado anauguza jeraha la mguu lakini Ilkay Gundogan na Toni Kroos wako imara baada ya kushiriki katika mechi ya Juni 7 ya kujipima nguvu dhidi ya Latvia.

Timu hizi mbili zilikutana katika Euro mwaka 2016 hatua ya nusu fainali na Ufaransa ikashinda 2-0, Antoine Griezmann akifunga mabao yote mawili.

Iwapo kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps atashinda taji hili la Euro mwaka huu, basi atakuwa mtu wa kwanza kushinda kombe la dunia na Euro akiwa mchezaji na kocha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.