Pata taarifa kuu
UEFA-ARSENAL-SOKA

Arsenal kuondoka UEFA na hatima ya Wenger

Baada ya klabu ya Arsenal ya Uingereza kuondolewa katika michuani ya klabu bingwa barani Ulaya na Barcelona ya Uhispania, kocha Arsene Wenger anakabiliwa na maswali mengi kuliko majibu kuhusu kuendelea kwake kuwa kocha wa klabu hiyo.

Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2014.
Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2014. REUTERS/Eddie Keogh
Matangazo ya kibiashara

Arsenal imeondolewa baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 5 kwa 1 nyumbani na ugeni. Wakiwa nyumbani vijana wa Wenger walifungwa mabao 2 kwa 0 na baadaye ugenini wakakubali kichapo cha mabao 3 kwa 1.

Nchini Uingereza, umekuwa ni msimu wa matumaini makubwa kwa Arsenal ambayo mwanzoni mashabiki wake walikuwa na matumaini kuwa huu ndio mwaka wa kunyakua ubingwa na kumaliza ukame wa zaidi ya miaka 10.

Pamoja na kwamba kuna matumaini ya Arsenal kumaliza katika nafasi ya nne bora na kufuzu tena katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mwaka ujao, suala ambalo mashabiki wanasema limekuwa la kawaida kwa klabu yao kila mwaka lakini hawaoni matunda ya hilo.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright amenukuliwa akisema kuwa, mashabiki wengi wa klabu hii wanamtaka Wenger kuondoka na wengi inavyoonekana wameshamchoka baada ya miaka 20 kuwa katika klabu hii.

Swali kubwa linaloulizwa na wengi hasa mashabiki, je Profesa Wenger ataendelea kuwepo msimu ujao ikiwa hatafanikiwa kunyakua ligi kuu ya soka nchini Uingereza ?

Vlabu vingine vikubw akama Chelsea, Manchester United, Manchester City na Liverpool tayari zimepitia kipindi kigumu hapo awali cha mabadiliko na hata kubadilisha makocha wake lakini hili halijashuhudiwa klatika klabu hii ya Arsenal.

Hili swala halijawakera tu mashabiki wa Arsenal lakini pia wachezjai wa zamani, mchezaji mwingien wa zamani Emmanuel Petit hivi karibuni alinukuliwa akisema huu ndio mwaka ambao klabu yake ya zamani ingenyakua ubingwa lakini inavyoonekana hili huenda lisitokeee.

Wapenzi wa klabu hii wanafahamu kuwa, Wenger amesaidia kunyakua mataji matatu ya klabu bingwa huko uingereza, na manne ya Shirikisho la soka FA hivi karibuni ikiwa ni mwaka 2014 na 2015.

Kuna wale wanaoona kuwa kusajiliwa kwa wachezaji kama Mesut Ozil na Alexis Sanchez kungeleta mwamko mya katika klabu hiyo lakini sera ya Wenger imeifanya klabu hii kutofanya vizuri has akatika michuano hii ya lala salama ya kuwania taji la Uingereza lakini pia kama ilivyodhihirika katika michuano ya UEFA.

Arsène Wenger, meneja wa Arsenal.
Arsène Wenger, meneja wa Arsenal. Reuters

Kwa heri Wenger

Mafanikio ya Wenger ya miaka 20 katika klabu hii hayawezi kupuuzwa hata kidogo.

Wenger mwenye umri wa miaka 66, amejijengea jina na heshima katika klabu hii lakini pia kusifiwa kwa fursa ya kuwapa vija auonesha vipaji vyao.

Mshikadau Mkuu wa klabu hii kutoka Marekani Stan Kroenke ameonekana kusikitishwa na matokeo ya Arsenal na kusikia kilio cha mashabiki na huenda wakati wa mwishi wa Wenger huko Emirates unafiki tamati.

Hii inaonesha kuwa, kilio cha mashabiki kinasikilizwa sana na hakiwezi kupuuzwa sana.Mashabiki wa Arsenal wanataka , mataji.Wamechoka na burudani.

Hivi karibuni kumekuwa na maandishi kama haya, hasa wakati klabu hii inapoecheza, #WengerOUT# katika mitando ya kijamii hasa Twitter.

Wengine, wamemshukuru Wenger kwa mazuri aliyowafanyia miaka 20 sasa na kusisitioza kuwa huu ndio wakati wa kusalimu amri na kumwachia mtu mwingine kujaribu kuisaidia klabu hii kunyakua ubingwa.

Arsenal imekuwa ni kama mtu anayekwenda katika sherehe, anaalikuwa kwenda kushiriki mashindano ya kucheza densi lakini yeye haoneshi juhudi zozote za kutaka kushinda.

Mchezaji wa zamani wa Mancheter United, Paul Scholes alinukuliwa akisema kitu cha mwisho ambacho angetaka kukukiona kwa kalbi yake ni kumaliza katika nafasi ya nne na kufuzu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kila mtu kufurahia hatua hiyo, badala ya kupambana kushinda ligi.

Arsenal imeonesha kuwa, inapomaliza katika nafasi ya nne na kufuzu katika michuano ya UEFA, basi mambo ni mazuri lakini wanaoumia ni mashabiki.

Miongoni mwa maswali ambayo Wenger anastahili kujiuliza baada ya kuondolewa katika michuano ya UEFA ni, ujuzi wangu umefika mwisho ?

Arsene Wenger (kulia) akificha macho yakebaada ya timu yake kuchapwa mabao 6-0 katika mchuano dhidi ya Chelsea.
Arsene Wenger (kulia) akificha macho yakebaada ya timu yake kuchapwa mabao 6-0 katika mchuano dhidi ya Chelsea. REUTERS/Eddie Keogh

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.