Pata taarifa kuu
ARSENAL-BAYERN-UEFA-SOKA

Arsenal yaburuzwa magoli matano na Bayern

Arsenal imeangukia pua baada ya kuchapwa mabao matano kwa moja la kufutia macho lililofungwa na Olivier Giroud katika dakika ya 69 za kipindi cha pili.

Meneja wa Arsenal, Arsène Wenger (kulia) akiinamisha macho yake chini baada ya timu yake kushindwa kufanya vizuri ikiwa nyumbani.
Meneja wa Arsenal, Arsène Wenger (kulia) akiinamisha macho yake chini baada ya timu yake kushindwa kufanya vizuri ikiwa nyumbani. REUTERS/Eddie Keogh
Matangazo ya kibiashara

Arsenal ilianza kunyeshewa mvua ya mago katika kipindi cha kwanza, ambapo kipindi hicho kimemalizika Bayern ikiwa na magoli matatu dhidi ya Arsenal ambayo ilikua ikiichezea nyumbani.

Mabao ya Bayern yamefungwa na Robert Lewandowski (dakika ya 10), bao aliloliingiza kwa kichwa, na katika dakika ya 29 Thomas Muller aliliona lango la Arsenal na kuweka kimyani bao la pili. Katika dakika ya 44, kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, David Alaba alihitimisha kwa kufunga bao la tatu, na hivyo kuwaweka Arsenal , wenyeji kwa mabao 3-0 hadi kufikia muda wa mapumziko.

Katika kipindi cha pili, Bayern ilikuja juu na kutawala mpira kwa pasenti kubwa. Katika dakika ya 55, Arjen Robben alifunga bao la nne katika kipindi cha pili, huku Muller akimaliazia bao kwa bao la tano katika dakika ya 89 na kukamilisha kichapo hicho.

Kwa sasa Arsenal wanakabiliwa na kibarua kigumu katika juhudi zao za kutaka kufuzu kwa hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupoteza mechi yake na Bayern.

Kushindwa kwa Arsenal na Bayern, kunapelekea klabu hiyo kuanguka, ikiwa imesalia na mechi mbili pekee, huku ikiwa na alama sita nyuma ya Bayern na Olympiakos.

Ushindi wa 2-1 wa klabu hiyo ya Ugiriki dhidi ya Dinamo Zagreb unamaanisha kwamba sasa Arsenal hawana usemi kuhusu uwezekano wao wa kufuzu na wamo hatarini ya kushindwa kufika hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza katika misimu 13.

Arsenal watahitaji kushinda mechi zilizosalia na waombe sana Olympiakos washindwe mechi zilizobaki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.